KAMATI HALMASHAURI YA UBUNGO ZAWASILISHA TAARIFA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA TATU JANUARI – MACHI 2018.

Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa robo ya tatu ya mwaka (Januari – Machi 2018) umefanyika mapema siku ya leo Ijumaa Mei 18, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Kibamba, ambapo kamati mbalimbali zimewasilisha taarifa zake. Katika Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti ambaye ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, jumla ya kamati tano zimeweza kuwasilisha taarifa zake. Kamati hizo ni pamoja na: Kamati ya Afya, Kamati ya Fedha na Uongozi, Kamati ya Maadili, Kamati ya Mipango Miji na Mazingira, na Kamati…

Soma Zaidi >>

KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI NA FAINALI ZA MAPEMA.

Zikiwa zimesalia siku 27 kuelekea nchini Urusi kwenye Kombe la Dunia,  nakuletea makala ya michezo mitano mizuri ya kutazama “Fainali za mapema”. Fainali ya kwanza itakuwa 15/6/2018. Katika dimba la Fisht kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya mabingwa wa 2010 wa kombe la dunia Hispania dhidi ya Ureno, waatalamu wa historia wanautaja huu mchezo kuwa ni mchezo wa mahasimu (derby )ni moja ya derby kwa timu za taifa kwani ukiacha tu mpira Hispania na Ureno zinatokea eneo moja la ulaya yaani Ulaya Magharibi ( lugha moja ),…

Soma Zaidi >>

MBUNGE ‘MOSHI MJINI’ ATUMIA BUNGE KUMKUMBUSHA RAIS MAGUFULI AHADI YA KM 10 BARABARA ZA LAMI

Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffary Michael  amelitumia bunge kumkumbusha Rais John Magufuli ahadi aliyoitoa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ya kujenga barabara yenye urefu wa km 10 kiwango cha rami katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi. “Ujenzi wa mtandao wa rami katika barabara ya Moshi inaridhisha, fedha hizo zilitolewa na mfuko wa barabara pamoja na benki ya dunia, hazina mahusiano na ahadi ya rais aliyoitoa kwenye kampeni kuhusu ujenzi wa km 10 za rami katika halmashauri ya Moshi,” amesema Safari. Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri…

Soma Zaidi >>

SPIKA NDUGAI ASHAURI WAHITIMU WA VYUO WALIOKOSA AJIRA KUGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewashauri wahitimu wa vyuo vikuu waliokosa ajira, kugombea nafasi za udiwani na ubunge. Spika Ndugai ametoa ushauri huo leo jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, ambapo amesema kazi hizo za kuwawakilisha wananchi hazihitaji uzoefu. “Kuna ajira nyingine hazihitaji uzoefu, kuna udiwani, ubunge. Najua nawatangazia vita watu wengine,” amesema Spika Ndugai. Ushauri huo umekuja baada ya Mbunge Viti Maalumu, Zainab Katimba kulalamika kwamba vijana wengi wanakosa nafasi za ajira kutokana na masharti ya nafasi za ajira zinazotelewa kuwabana…

Soma Zaidi >>

WHO YAITISHA MKUTANO WA DHARULA KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI EBOLA KUTOKA DRC CONGO

Shirika la Afya Duniani-WHO linandaa mkutano wa dharula kujadili hatari ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola kutoka katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mkutano huo unafanyika leo ambapo jopo la washiriki wake wataamua iwapo hali ya dharula itatangazwa ili kuongeza muitikio mkubwa kwa jamii za kimataifa katika kukabiliana na ugonjwa huo. Hadi sasa watu takribani 44 wanaaminika kuambukizwa na mlipuko wa ugonjwa huo huku vifo vya watu 23vinachunguzwa. Ebola ni ugonjwa unaoambukiza unaosababisha kuvuja damu ndani ya mwili na mara nyingi waathiriwa hufariki. Unaweza kusambaa kwa haraka kwa…

Soma Zaidi >>

AHADI YA MIL. 50 KILA KIJIJI YAIBULIWA BUNGENI, MBUNGE AITAKA SERIKALI KUELEZA ITATEKELEZA LINI

Mbunge wa Jimbo la Konde, Hatibu Haji (CUF)  ameiibua ahadi ya milioni 50 kutolewa kwa kila kijiji iliyotolewa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ambapo aliihoji serikali kama imeshindwa kuitekeleza na kama haijashindwa itazitoa lini fedha hizo kwa wananchi. HatibU ametoa hoja hiyo leo Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, ambapo ilijibiwa na Naibu waziri ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira, Anthon Mavunde. “Rais katika kipindi cha uchaguzi sera yake ilikuwa kutoa milioni 50 kila…

Soma Zaidi >>

MBUNGE ATOA KALI YA MWAKA, ASHINDWA KUULIZA SWALI BUNGENI KISA MWEZI WA RAMADHANI

Mbunge Viti Maalumu anayewakilisha kundi la vijana bungeni, Khadija Nasiri Ali amesema ameshindwa kueleza masikitiko yake pamoja na kuuliza swali bungeni kwa sababu ya mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani. Hadija ameyasema hayo leo katika kipindi cha maswali na majibu baada ya kutoridhishwa na majibu ya serikali kuhusu swali lake alilouliza namna mfuko wa vijana ulivyosaidia wananchi kujikwamua kiuchumi. “Majibu yako kisera zaidi, kwa vile niko katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, nashindwa kueleza masikitiko yangu,” amesema Hadija. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde amesema…

Soma Zaidi >>

SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI AMWANDIKIA BARUA SPIKA NDUGAI

Spika wa Bunge la Afrika la Mashariki-Eala,  Martin Ngoga amemuandikia barua Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akitoa pongezi kwa bunge hilo kwa maandalizi mazuri ya mkutano wa 4 uliofanyika kuanzia Aprili 8 hadi 27, 2018 katika ukumbi wa Msekwa ulioko bungeni jijini Dodoma. Hayo yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Spika Ndugai wakati akitoa taarifa mbalimbali kwa wabunge. “Spika wa Bunge ameniandikia barua kutoa shukrani za dhati kwa maandalizi mazuri yaliyopelekea mkutano kufanyika na kufanikiwa vizuri,” amesema Spika Ndugai. Aidha, Spika Ndugai aliwashukuru wabunge na wadau…

Soma Zaidi >>

RAIA WA KIGENI 129 WADAKWA WAKIOMBA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Raia wa kigeni takribani 129 wanashikiliwa mkoani Kigoma kwa kosa la kuingilia mchakato wa uandikishaji vitambulisho vya taifa. Watu hao wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji wasio rasmi walikamatwa katika zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho ambapo walijitokeza kushiriki. Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti alithibitisha taarifa hizo jana alipotembelea kituo cha Murusi ambapo walifika kujiandikisha ili wapate vitambulisho hivyo. “Tumewashikilia watu hao kwa ushirikiano wa wananchi na maofisa uhamiaji. Niwaombe wale wote ambao si raia mjitokeze kabla hatujaanza kuwabaini,” alisema Jenerali Gaguti.…

Soma Zaidi >>

HABINDER SETHI AWA MBOGO KUVULIWA UENYEKITI IPTL

Mmiliki wa Kampuni ya Kampuni ya PAP/IPTL,Harbinder Sing Sethi amekanusha taarifa zinazosambzwa mitandao kuwa amefutwa kuwa Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo. Hayo yalielezwa jana na Mwanasheria wa mmiliki wa Kampuni ya PAP/IPTL, Harbinder Sing Sethi, Hajra Mungula,  kupitia taarifa yake kwa umma mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mteja wake na kusema Sethi bado Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo. Taarifa hiyo iko chini.  

Soma Zaidi >>