NJOMBE MJI WAIDUWAZA NDANDA FC, MBEYA CITY NA SINGIDA UNITED, WATHIBITISHA UBISHI WAO.

Michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) imemalizika jioni hii katika viwanja viwili tofauti, ambapo huko Njombe timu ya Njombe Mji imewafundisha soka vijana kutoka Mtwara Kuchere, Ndanda FC, na huko mkoani Mbeya timu za Mbeya City na Singida United zimeonyesha ubabe wao. Tukianza na matokeo katika mji wa Njombe, timu ya njombe Mji imefanikiwa kuilaza timu ya Ndanda FC kwa jumla ya bao 2-0, magoli yaliyofungwa na mchezaji Notker Masasi katika dakika ya 17 na Amhed Adewale katika dakika ya 50 ya mchezo. Huko katika dimba la Sokoine…

Soma Zaidi >>

BODI YA FILAMU KENYA (KFCB) KAMA BASATA.

Ikiwa hapa nchini Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, imekuwa ikipiga vita shughuli zote za kisanaa ambazo ni kinyume na maadili ya Tanzania, nayo nchi ya Kenya imeamua kulivalia njuga suala hili.   Huko nchini Kenya, Bodi ya Filamu ya Kenya (KFCB) imepiga marufuku filamu zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya nchi hiyo, huku ikishusha rungu lake kwa filamu mpya nchini humo iitwayo ‘Rafiki’, ambayo imepigwa marufuku kuchezwa nchini humu.   Filamu hiyo inadaiwa kugusua masuala ya jinsia moja, kitendo…

Soma Zaidi >>

UVCCM DODOMA YAPONGEZA UAMUZI WA RAIS MAGUFULI WA KUITANGAZA DODOMA KUWA JIJI.

Dodoma. Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Dodoma, umepongeza uamuzi wa Rais Magufuli wa kuitangaza Manispaa hiyo kuwa Jiji. Pongezi hizo zimetolewa mapema siku ya leo, na Mwenyekiti wa Umoja huo, Billy Chidabwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ameipongeza hatua hiyo ya Rais na kusema kuwa ilikuwa ni shauku ya muda mrefu ya wana Dodoma kuona mji huo ukipandishwa hadhi, kutoka kuwa Manispaa hadi kuwa Jiji. Mapema siku ya jana April 26, 2018, kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na…

Soma Zaidi >>

BAADA YA KUHARIBU MIPANGO YA YANGA, LEO NI ZAMU YA SINGIDA UNITED, SOKOINE MBEYA.

Ligi Kuu Tanzani Bara jioni hii inaendelea katika dimba la Sokoine mkoani Mbeya, ambapo wabishi wa Mbeya City wanawakaribisha walima alizeti wa Singida United kutoka mkoani Singida. Katika mchezo wake uliopita timu ya Mbeya City iliilazimisha sare ya bao 1-1 timu ya Yanga, ambayo ilikuwa imepania kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake. Je leo matokeo yatakuwaje kati ya timu hiyo na Singida United ambao nao wameonekana kuwa timu ngumu yenye kuvisumbua vigogo hapa nchini, ambapo katika mechi zake zote za ligi kuu, Singida imefanikiwa…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAELEZA MIKAKATI YAKE KATIKA KUZUIA UVUVI HARAMU NCHINI.

Dodoma. Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imeeleza mikakati ayke ambayo imekuwa ikiichukua ili kupambana na shughuli za uvuvi harama hapa nchini. Mikakati hiyo imeelezwa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah  Ulega,  alipokuwa akijibu swali la Mbunge Hamida Mohamed Abdallah (Viti Maalumu) aliyetaka kujua ipi ni mikakati ya seriakali katika kukabiliana na uvumi haramu hapa nchini. “Mwaka 1974 Tanzania iliridhia Mkataba wa Kuzuia Uchafuzi wa Bahari na Usalama wa Bahari ambao lengo moja wapo ni kuzuia uvuvi haramu wa…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA KONDOA – BABATI, MAARUFU KAMA THE GREAT NORTH.

Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Ijumaa ya leo April 27, 2018, amezindua barabara ya Kondoa – Babati, maarufu kama ‘The Great North’. Mhe. Rais amefanya uzinduzi huo katika mji wa Bicha wilayani Kondoa, ambapo amesema barabara hiyo itasaidia kurahisisha shughuli za maendeleo kwa wakazi wa maeneo hayo na mikoa ya jirani, huku akisisitiza matumizi mazuri ya barabara hiyo na katu wananchi wasijaribu kuharibu alama za barabarani zilizowekwa kwenye barabara hiyo. Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi wengine wa kimataifa na kitaifa, akiwemo…

Soma Zaidi >>

JOHN HECHE ASEMA WATU HAWAKO SALAMA TENA MIKONONI MWA POLISI,NI BAADA YA MDOGO WAKE KUUAWA

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), mheshimiwa John Heche, amesema mdogo wake anayejulikana kwa majina ya Suguta Chacha, ameuuawa kwa kuchomwa kisu na polisi wa kituo cha Sirari usiku wa kuamka leo. Mbunge huyo amedhibitisha kuuawa kwa ndugu yake huyo katika ujumbe wake kwenye ukarasa wake wa mtandao wa Twitter kuwa leo Aprili 27 2018 na kusema kuwa Suguta alichomwa kisu na polisi waliomkamata baada ya kumkuta baa akinywa pombe. Inadaiwa polisi wametekeleza tukio hilo huku akiwa na pingu mkononi. “Watu hawako salama tena mikononi mwa polisi. Mdogo wangu Suguta…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI AAGIZA WALIOFANYA UBADHIRIFU WA BIL.1.5 ZA MRADI WA MAJI WATUMBULIWE

Rais John Magufuli ameagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu waliofanya ubadhirifu wa kiasi cha Sh. Bilioni 1.5 katika mradi wa maji kwenye wilaya za Chemba na Kondoa. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo katika sherehe za uzinduzi wa barabara ya Kondoa kwenda Babati iliyofanyika wilayani Kondoa mkoa wa Dodoma. Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge kusema kuna ubadhirifu wa bilioni 1.5 kwenye mradi huo. “Wakati mwingine sisi viongozi tunatakiwa kuchukua hatua hata kama zinauma kwa manufaa ya watanzania wengine,” amesema…

Soma Zaidi >>