MKUTANO MKUU WA KLABU YA SIMBA KUFANYIKA DESEMBA 3, MWAKA HUU.

Klabu ya Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es Salaam, inatarajia kufanya Mkutano wake Mkuu Maalum wa klabu, utakaofanyika Jumapili ya Desemba 3, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo kwa Waandishi wa Habari, imeeleza kuwa agenda za mkutano huo zitasambazwa kwa wanachama wote wa matawi ili kuwafikia wanachama wote wa Klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi. Aidha, Kamati hiyo imewataka wanachama wote wa Klabu ya Simba, kuhudhuria kwa wingi kwenye…

Soma Zaidi >>

WAANDAMANAJI WAWILI WAUWAWA NA POLISI JIJINI NAIROBI

Msafara wa kiongozi wa upinzani nchini Raila Odinga baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kutoka Marekani Takriban watu wawili wameuawa katika mji mkuu wa Nairobi huku maafisa wa polisi wakikabiliana na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga . Gari moja la maafisa wa polisi pia lilichomwa . Makundi ya watu yalikusanyika katika uwanja wa ndege kumkaribisha kiongozi huyo amabye alikuwa amerejea kutoka mataifa Marekani. Raila Odinga alisusia marejeleo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti. Kulikuwa na ripoti za maafisa wa polisi waliorusha vitoa machozi katika…

Soma Zaidi >>

SPIKA NDUGAI AUNDA KAMATI KUCHUNGUZA SEKTA YA UVUVI NA GESI

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameunda kamati mbili zitakazoshughulikia sekta ya uvuvi wakuu na gesi akisema lazima wajue ni kwa nini hazichangii pato la Taifa. Ndugai ameunda kamati hizo baada ya zingine mbili za kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilisha taarifa kwa Rais John Magufuli Septemba,2017 na kusababisha baadhi ya mawaziri kujiuzulu. Akitangaza kamati za sekta ya uvuvi na gesi bungeni mjini Dodoma leo Ijumaa Novemba 17,2017, Spika Ndugai amemrejesha Dotto Biteko aliyeongoza kamati iliyochunguza Tanzanite kuwa mwenyekiti wa kamati itakayochunguza…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA MADINI

  Serikali kupitia Wizara ya Madini, imewakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza kwenye miradi mbali mbali ya madini hapa nchini. Wito huo ulitolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke na ujumbe alioambatana nao Wizarani hapo kutoka kwenye Ubalozi huo ili kujadiliana masuala mbalimbali ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji.   Waziri Kairuki alisema kuwa, Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini na hivyo zipo fursa lukuki za uwekezaji ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za…

Soma Zaidi >>

SERIKALI KUIMARISHA TTCL ILI KUFIKIA USHINDANI KIBIASHARA

Serikali ya Tanzania imedhamiria kuimarisha Kampuni ya Simu nchini (TTCL) iIi iweze kuingia kwenye ushindani wa kibiashara dhidi ya makampuni mengine ya simu. Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Kindamba alisema hayo kufuatia Novemba 14, mwaka huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadili na kupitisha miswada ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yanayofuta sheria iliyounda Kampuni ya Simu ya TTCL (Tanzania Telecomunication Company, Incoporation Act 2002) na kutunga sheria…

Soma Zaidi >>

JICA YASAINI MAKUBALIANO NA SERIKALI KUSAIDIA SEKTA YA UMEME NCHINI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Joseph Kakunda anayeshughulikia Elimu, Maji, Kilimo, Mifugo na Maliasili, amefungua Mkutano wa kwanza wa kazi kwa Kaimu Makatibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) katika ukumbi wa chuo cha Mipango mjini Dodoma leo. Mkutano huo ni wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Tume ya TSC mwaka 2015, ambao hutakiwa kufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa malengo mbalimbali likiwemo kupitia kanuni, sheria na taratibu za Tume hiyo. Akifungua kikao kazi hicho mjini Dodoma, ameagiza kuwepo kwa ushirikiano baina ya TSC, Idara…

Soma Zaidi >>

MWENYEKITI WA ALAT NA MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA ATOA MSAADA WA PAMPU YA MAJI KATA YA CHIBE

Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam ametoa msaada wa pampu ya maji na mifuko 10 ya saruji vyenye thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji katika kitongoji cha Mwamapalala kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga. Mukadam amekabidhi msaada huo wa pampu ya maji na mifuko ya 10 ya saruji kwa diwani wa kata ya Chibe John Kisandu leo Ijumaa Novemba 17,2017 kwa ajili ya mradi wa…

Soma Zaidi >>

RAIS MUGABE AONEKANA HADHARANI KWA MARA YA KWANZA

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano wiki iliyopita. Mara baada ya kuruhusiwa kutoka kizuizini kwa siku kadhaa, rais Mugabe aliweza kuhudhuria sherehe za mahafali katika Chuo Kikuu kimoja kwenye Mji Mkuu wa nchi hiyo Harare. Ikumbukwe kuwa, rais huyo mwenye miaka takriban 93, amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi kiti chake cha urais. Taarifa iliyotolewa na Jeshi la nchi hiyo, ilieleza Ijumaa iliyopita…

Soma Zaidi >>

DAWA YA DENI KULIPA -MKURUGENZI BENCH MARK PRODUCTIONS

Na Sabina Wandiba Mwanamke wa kwanza kuleta mifumo ya digitali hapa nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bench Mark Production, Rita Pousen (Maddam Rita) ametoa ufafanuzi kuhusiana na madai ya kufirisiwa kwa kampuni hiyo ambayo ilikuwa inadaiwa kodi na Mamlaka ya Mapato nchini TRA. Maddam Rita ametoa ufafanuzi huo muda mchache uliopita alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja na Televisheni kufuatia kuwepo kwa tetesi za kufirisiwa kwa kampuni hiyo kubwa. Alipotakiwa kutolea ufafanuzi kuhusiana na madai hayo, Maddam Rita alisema kuwa, kwa kawaida lazima kutambua kuwa dawa ya deni ni kulipa…

Soma Zaidi >>

MNYAMA ATAWATAFUNA MAAFANDE WA TANZANIA PRISONS MBEYA?

  Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara VPL inatarajia kuendelea tena kesho huku viwanja kadhaa katika miji tofauti vikiwaka moto ingawa macho mengi yataelekezwa kule Sokoine stadium Mbeya ,ambapo vinala wa ligi hiyo klabu ya Simba ya dar es salaam itashuka dimbani kukipiga na maafande wa Tanzania prison ambao msuli wao umeonekana kua imara zaid msimu huu wakinusa nafasi tano za juu katika msimamo huo. Mchezo huo unaotarajia kuwa wakusisimua kutokana na ubora wa klabu zote mbili kuanzia mabechi ya ufundi mpaka uwanjani pia nafasi katika msimamo wa ligi utakua…

Soma Zaidi >>