WAJASIRIAMALI NJOMBE WAPEWA DARASA KUFIKIA MAFANIKIO.

Na, Amiri kilagalila Wajasiriamali Mkoani Njombe wametakiwa kuzingatia kanuni za Kibiashara ikiwemo kulinda Mitaji yao ili kuhakikisha Mitaji inabaki salama bila kufilisika kutokana na Wajasiliamari wengi kufanya kazi Bila kuzingatia kanuni za Kibiashara na Mwisho hujikuta wamefilisika. Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la General Bussness Company Limited Alexander Malya jana januari 17 alipokuwa akitoa Mafunzo ya Ujasiriamali katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa baadhi ya wakazi Mjini Njombe ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakishindwa kukua kutokana na Kutofuata kanuni za Kibiashara. Pamoja…

Soma Zaidi >>

WAZIRI BITEKO, PROF.MSANJILA WAUTAKA MGODI WA NORTH MARA KUTII MAMLAKA ZA SERIKALI

Waziri wa Madini Doto Biteko pamoja katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof.Simon Msanjila wakutana na uongozi wa mgodi wa North Mara na kuutaka kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo. Akizungumza katika kikao kilichofanyika tarehe 17 Januari, 2019 katika Ofisi ya Waziri jijini Dodoma, Biteko aliwaeleza wajumbe hao kuwa walipaswa kuwa wamechukua hatua kadhaa kuonesha kua wanatii maagizo ya Serikali lakini kutokana na wao kuhisi serikali haina cha kufanya wakaamua kutulia kwa miezi mine ambapo wamefika Ofisini kueleza masuala ambayo hayajafanyiwa kazi. Hatuwezi kuwa tunakaa, tunafikia maamuzi ninyi…

Soma Zaidi >>

WAFANYABIASHARA DODOMA HATARINI KUPATA MAGONJWA

Wafanyabiashara na watumiaji wa soko la sabasaba lililopo jiji la  Dodoma wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kutokana na mlundikano wa uchafu uliopo ndani ya soko hilo. Akizungumza kwenye eneo hilo la dampo na waandishi wa habari mjumbe wa uogozi wa mpito soko hilo,Mabewo Daudi alisema kuwa mlundikano huo unatokana na jiji kutoondoa uchafu huo kwa wakati na kusababisha kuwepo pia kwa harufu kali. Aidha alisema kuwa kuwepo kwa uchafu huo kunaweza kuhatarisha mlipuko wa magonjwa ya tumbo kwa wafanyabishara wenyewe na hata kwa watumiaji wa…

Soma Zaidi >>

WAZAZI NGARA WAPEWA SIKU 14 KUWAPELEKA SHULE WATOTO WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA

Na Mwandishi wetu Ngara Mkuu wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele ametoa muda wa siku 14 kwa wazazi na walezi wilayani humo kuhakikisha wanawapeleka shule wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kabla ya kuanza msako wa nyumba kwa nyumba. Mntenjele ametoa muda huo hii leo baada ya kizindua ujenzi wa vyoo vyenye jumla ya matundu 12 na tanki moja la Maji katika shule ya sekondari ya Kabanga wilayani Ngara vilivyojengwa na shirika la Tumaini fund chini ya kanisa la Anglikana dayosisi ya Kagera kupitia kwa…

Soma Zaidi >>

MWENYEKITI CCM TARIME APIGA TAFU UJENZI WA SHULE SHIKIZI

Na Frankius Cleophace Tarime. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime mkoani Mara Daud Marwa Ngicho ametoa kiasi cha shilingi milioni moja, mifuko 50 ya saruji na lori tano za mchanga kwa ajili ya kuunga nguvu za wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Keweirumbe iliyopo katika kijiji cha Masurura kata ya Goronga wilayani humo ili kupunguzia wanafunzi hao kutembea zaidi ya kilometa 600. Mwenyekiti huyo amedai kuwa ameamua kuchangia ujenzi huo baada ya kuona nguvu za wananchi katika ujenzi huo kuwa kubwa na kuonyesha nia na moyo…

Soma Zaidi >>

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAKAA YA MAWE NA CHUMA LIGANGA KUANZA RASMI.

Na, Mwandishi wetu Wizara ya Madini imesema itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kuweka msukumo ili kuhakikisha kwamba miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na ule wa Chuma Linganga inaanza kutekelezwa. Kauli hiyo ilitolewa Januari 16 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za madini mkoani Njombe na kuona namna ya kutatua changamoto zinazohusu Wizara ya Madini katika utekelezaji wa miradi hiyo. Alisema miradi hiyo ni moja ya miradi ya kimkakati ambayo Taifa linatarajiwa…

Soma Zaidi >>

SUALA LA POLISI KUWAVIZIA NA KUWAFUKUZA BODABODA KAGERA SASA BASI.

Na: Mwandishi wetu-Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti aweka wazi mikakati yake ya kuwafanya Waedesha Pikipiki maarufu kama Bodaboda Mkoani Kagera hasa katika Manispaa ya Bukoba kuwa mojawapo ya Utalii katika Mji wa Bukoba na bodaboda hao kufanya kazi zao kiueledi na kwa kuinua vipato vyao huku wakijishughulisha na ujasiliamali katika vikundi vyao. Ni baada ya Mkuu wa Mkoa Gaguti kukutana na Bodaboda katika Ukumbi wa Linas Night Club Manispaa ya Bukoba Januari 17, 2019 na kuongea nao ambapo aliweka wazi ni jinsi gani atahakikisha…

Soma Zaidi >>

OPARESHENI YA UKUSANYAJI MAPATO JIJI LA ARUSHA YAANZA UPYA

Na.Fatuma S Ibrahimu – Arusha Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni amesema kuwa ifikapo kesho Tarehe 18 Januari, 2019 operesheni ya ukusanyaji wa mapato inatarajiwa kuanza upya baada ya kupumzika kwa muda mfupi kupisha msimu wa mapumziko na sikukuu. Ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake leo Taehe 17 Januari, 2019 ambapo ameitambulisha timu mpya katika awamu hii ambayo ni Wakuu wa Idara zote zilizoko Halamshauri ya Jiji la Arusha na kila mmoja ataambatana na watumishi walio chini yake na watapangiwa maeneo…

Soma Zaidi >>

MATUKIO YA MAUAJI NJOMBE YANAHUSIANA NA USHIRIKINA:KAMANDA NGONYANI

Na Amiri kilagalila Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limezungumza na waandishi wa habari Kufuatia matukio ya utekaji, kujeruhi na mauaji yaliyoibuka hivi karibuni mkoani Njombe ambapo pamoja na kuthibitisha uwepo wa matukio hayo jeshi hilo limesema yanatokana na imani za kishirikina kwa asilimia kubwa. Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo katika Ofisi za polisi makao makuu ya polisi mkoani Njombe kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Rashid Ngonyani amesema kuwa matukio hayo kwasasa yametawala zaidi katika Eneo la Njombe mjini ambapo wahanga wakubwa wa Matukio hayo…

Soma Zaidi >>