ZOEZI LA UHAKIKI.. LIFIKIE TAMATI SASA, WATUMISHI WAPATE STAHIKI ZAO.., MAISHA YAENDELEE ;

© Martin Maranja Masese

.., kwa akili yangu timamu sana.., naweza kusema kwamba serikali yangu inacheza na akili zetu zilizo timamu.., huu uhakiki wa kila kila siku kwa mwaka mzima sasa.., ni kutafuta namna ya kuchelewesha watumishi wenye sifa za kupanda daraja wasipandishwe madaraja, wahitimu wenye sifa za kupata ajira rasmi, wasipate ajira, kupandisha mishahara kwa mujibu wa mikataba ya ajira nk.

…, binafsi nimekua na wasiwasi sana.., sifikirii kama zoezi hili linafanywa Kwa weledi uliotukuka.., (naiona mitupio ya kisiasa kwenye suala hili).., hauchelewi kusikia kwamba sekta kadhaa ndiyo zinazoongoza Kwa watumishi hewa wakati zipo sekta ambazo hausikii kamwe zikiguswa na uhakiki huu kabisa …na pengine huenda ndiyo zikawa na wafanyakazi wachache wenye kuchukua mamilioni Kwa mwezi na wengi walio hewa!

Uhakiki wa aina ipi hiyo unafanyika mwaka mzima?? Tena kwa nyenzo na namna ile ile, ukibadilishwa majina ya taasisi za ukaguzi tu.., Maana tangu mwezi machi mwaka huu, serikali inahangaika na kufanya uhakiki na ukaguzi.., ajira zikiwa zimesitishwa, kupandishwa madaraja kumesitishwa, inclement ya mishahara imesitishwa…

JPM alisema anataka mwezi mmoja hadi miwili ya uhakiki tamgu mwezi machi mwaka huu.., hiyo miezi 2 ikamakizika, akapelekewa taarifa na wizara ya utumishi iliyoko ofisini kwake.., siku chache baadae tunasikia tangazo lingine la uhakiki kabambe!

.., Uhakiki wa awali ulifanyika kati ya tarehe 05 hadi 15/09/2016 hapo ni baada ya ile miezi miwili ya awali ambayo aliitoa JPM kumalizika.., (ukumbuke uhakiki wa tangu awali ni agizo la JPM la tangu 15-03-2016)

tarehe 26/08/2016 ndiyo ilikuwa siku rasmi ya JPM kukabidhiwa taarifa kutoka katika menejimenti ya utumishi wa umma kuhusu watumishi hewa.., baada ya kupokea ndiyo akatoa miezi mingine miwili ya kuendelea na zoezi..

…, Tarehe 02-10-2016 ukatangazwa uhakiki mwingine tena.., uhakiki wa watumishi wa umma nchi nzima.., uhakiki wa kujiandikisha vyeti na kila kitu kwa kile kilichoitwa Uhakiki wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA)…, hivyo huu unaitwa UHAKIKI WA NIDA..

…, kitu cha ajabu sana.., wakati huo uhakiki bado unaendelea haujamalizika na hata kufika nusu, tarehe 05-10-2016 serikali ikatangaza tena uhakiki mpya ulioitwa UHAKIKI WA NECTA… tarehe 11-10-2016..,

.., najiuliza maswali kadhaa hapa, sipati jibu.., naishia kutikisa kichwa tu.., hivi serikali na taasisi zake zote, NIDA, NECTA, UTUMISHI, wameshindwa kumaliza suala hili kwa mwaka mzima!!!? Kwanini wanakiuka misingi ya mikataba ya ajira ya watumishi wa umma..!?

Kwa sababu kuna watumishi wanatakiwa kupandishwa madaraja, kuna watumishi wanatakiwa kubadilishwa data zao za mishahara ili waanze kupokea mishahara mipya, kuna wahitimu wako mtaani mwaka wa pili sasa.., hawana ajira na wanasubiri zoezi la uhakiki likamilike ili waajiriwe..,

Yaani cheti kimoja cha chuo, kidato cha 4 na kidato cha sita kinakaguliwa kwa mwaka mzima!? Halafu…, hizo gharama za nauli kwa watumishi wa umma nani anagharamia!!? Fikiria.., mtumishi anafanya kazi manispaa ya Ilemela, Mwanza lakini yuko masomoni TEKU (Theofile Kisanji University) Mbeya, nauli ni Tsh 60,000/- kwa basi, kwenda na kurudi ni Tsh 120,000/- (sasa jumlisha na safari zote za uhakiki alizotakiwa kuwepo kituoni)

.., kweli serikali haifahamu hilo suala la gharama au!? Hebu waajiri kuweni na huruma na watumishi wenu.. Haki za mtumishi akiwa nje ya kituo zilindwe (endapo ana ruhusa ya kiofisi kutoka kwa mwajiri au mkuu wa kituo au mkuu wa idara)..

Zoezi la uhakiki sasa lifike tamati, watumishi wa umma waendelee kupata stahiki zao kwa mujibu wa sheria za ajira na mikataba yao ya ajira.., wahitimu walioko mtaani wenye sifa za kuajiriwa na wanasubiri zoezi hili ili waajiriwe, watimiziwe matakwa yao pia..

KUHUSU UKAGUZI NA UHAKIKI WA VYETI; serikali ihakikishe imefika kwenye sekta zote za umma bila kubagua au kuchagua, zoezi hili lifanyike kwa weledi ili tibali na watumishi wenye uhitaji kamili wa sifa stahiki.., ukaguzi usiache chembe ya dosari, ufanyike ili mambo my mengine yaendelee..

…, nihitimishe kwa kusema kwamba, Kinacholigharimu taifa ni UTUNZAJI NA UBORESHAJI WA TAARIFA ZA WATUMISHI…,kuna utengano mkubwa ni baina ya wakurugenzi (ambao kimsingi ni waajiri wa sehemu kubwa ya watumishi) na Hazina…, mfumo wa data Base wa taifa letu hauko timamu, usishangae mtumishi kuombwa barua ya ajira au kuthibitishwa kazini halafu ofisi haina ‘hard copy’ au ‘soft copy’ ya barua hizo!

Kama ni kweli kuna ‘vyeti feki’ basi Tanzania inamhitaji Daudi wa kupambana na Goliati/Jairuti( Vyeti feki)…, vinginevyo hii ni SIHASA za SIASA (business as usual).., zoezi la zima moto kutafuta uungwaji mkono kuelekea 2020!

 

© Martin Maranja Masese [MMM]

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.