ZITTO ASIKITISHWA NA MGOMO WA WAFANYABIASHARA KIGOMA

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo ambaye pia ni mbuge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe ameonesha masikitiko yake juu ya mgogoro wa wafanyabiashara wa Masoko ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kuhusu tozo ya Pango.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mapema leo Desemba 30, Zitto ameonekana kuwashangaa wafanyabiashara wanaolalamikia kupanda kwa tozo la vibanda kutoka 15,000 hadi 50,000, akidai tozo hiyo ni ya kawaida sana. “Nikweli kuwa tozo ni kubwa sana kutoka 15,000 mpaka 50,000. Lakini tozo hii ni kubwa kulinganisha na nini?”, alihoji Mhe. Zitto.

Zitto anaendelea kwa kusema tozo ya 15,000 iliyokuwa ikitozwa mwanzo kwa wafanyabiashara wa manispaa ya Kigoma ilikuwa ndio tozo ndogo zaidi ukilinganisha na zoto zinazotolewa katika maeneo mengine ya Tanzania.

Katika andiko lake hilo, Mhe. Zitto amedai mchakato wa kupandisha tozo hiyo ulifuata taratibu na hatua zote, hivyo kuwasihi Wafanyabiashara kulipa tozo mpya iliyopangwa ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika manispaa hiyo kwani bajeti pekee ya serikali haitoshi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.