YONDANI AREJEA,JUMA MAHADHI MAMBO BADO MAGUMU

Daktar wa kikosi cha Young Africas Dk.Edward Bavu amethibitisha mchezaji Kelvin Yondani amepona majeraha yake na siku ya jana Jumatano ameanza rasmi mazoezi.

Yondani alipata majeraha akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambapo majeraha hayo yamfanya aondolewe katika kikosi cha timu ya Taifa kilichokwenda nchini Uganda.

Yondani anatarajiwa kuwa sehemu ya Kikosi cha Yanga kitakachoumana dhidi ya Standi United Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Saa 10:00 Jioni.

Aidha Dk.Edward Bavu amesema wachezaji wengine waliokuwa majeruhi na siku ya jana walianza kufanya mazoezi pamoja na Abdallah Sheibu Ninja na Juma Abdul,  mchezaji Juma Mahadhi akiwa bado ni majeruhi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.