YANGA YAKWEA PIPA YAIFATA TANZANIA PRISONS MCHANA KWEUPEE

Na Shabani Rapwi, Dar es Salaam.

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara siku ya Alhamis dhidi ya JKT Tanzania na kupata ushindi wa magoli 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga SC mchana wa leo Disemba 01, 2018 kimekwea pipa Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) kuelekea jijini Mbeya kwaajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Jumatatu Disemba 03 mwaka huu katika dimba la Sokoine mkoani Mbeya.

Ikumbukwe kuwa Yanga ndiyo vinara wa Ligi kuu Tanzania ikiwa na Pts 35 ikifatiwa na Azam FC yenye Pts 33 huku mabingwa watetezi Simba SC wakiwa na Pts 27 ikiwa na mchezo mmoja wa kiporo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.