WILAYA YA KILOLO KUNG’ARISHWA KWA BARABARA ZA LAMI

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mh. Asia Abdallah amewataka wananchi wa Kilolo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa barabara za lami katika wilaya hiyo unaotokana na juhudi za mbunge wa jimbo la kilolo, Mh. Venance Mwamoto pamoja na serikali ya awamu ya tano utakaondoa changamoto ya usafiri kwa wakina mama wajawazito, wazee na watu wa Kilolo.

“kwa hiyo watu watakapo kuja site tuwape ushirikiano wa asilimia 100 barabara itengenezwe na sisi tupate maendeleo kama wenzetu wa kule kaskazini walipofikia, sasa lami inakuja, Mh. Mbunge, mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewapigania kuhakikisha kuwa mnapata barabara ya lami ili tuanze kufanana na mikoa ya kaskazini kimaendeleo”

Hayo aliyasema katika mkutano na wananchi wa kata ya Kidabaga wakati wa kutia saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya lami unaotekelezwa kwa fedha za wahisani kutoka umoja wa Ulaya (EU) na shirika la maendeleo la Marekani (USAID

Naye mhandisi wa kitengo cha mazingira TARURA Makao makuu, Eng. Dkt. Veronica Mirambo amesisitiza kuwa barabara zinazotazamwa katika mradi ni zile zilizokatika maeneo ya kilimo cha umwagiliaji ambapo wilaya ya Kilolo ikitarajiwa kuwa na barabara ya lami kutoka Kidabaga hadi Boma la Ng’ombe yenye kilomita 18.3 na ile itakayounganisha wilaya ya Kilolo na halmshauri ya wilaya ya Iringa.

Eng. Mirambo ametaja kiasi cha euro milioni 46 zilizogawanywa katika vipindi vya miaka mitatu mfululizo kuanzia 2018-19, 2019-2020 na 2020-21 huku miongoni mwa barabara zitakazofaidika na mradi zikiwa ni ile za kutoka Inyara hadi Simambwe ya Mbeya  DC, kilomita 16.7, barabara ya Masebe hadi Mkuguso kilomita 50 na Masebe hadi Lutete, kilomita 7.2 zote kutoka Rungwe DC.

Akizungumza katika mkutano huo, Afisa maendeleo ya jamii TARURA Makao makuu, bi. Joha Rashid amesisitiza kuwa TARURA inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayotaka kuundwa kwa vikundi vitakavyopewa mafunzo ya utengenezaji na utunzaji wa barabara ili kutengeneza ajira mpya. 

“Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015 kifungu cha 3 kinasema kuundwa kwa vikundi vya mafundi wa barabara watakaofanya kazi ndogo ndogo kama kufyeka, kuzibua mitaro, kuweka viraka na kuzibua makaravati lengo kuu ikiwa ni kusaidia kupunguza umasikini”

Bi. Joha Rashid aliongeza kuwa ipo haja ya wananchi katika maeneo yote nchini kuunda vikundi vitakavyopewa mafunzo ya utunzaji wa barabara kwa ajili ya kulinda barabara zote kwa kuwa ni zao na si za serikali pekee kama ilivyodhana ya wananchi wengi nchini

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Kilolo, Mbunge wa jimbo hilo Mh. Venance Mwamoto amewataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika kazi zote zitakazojitokeza katika siku zote za mradi huku akiahidi wananchi wa jimbo hilo kupatiwa mafunzo katika vikundi yatakayowawezesha kufanya kazi hizo.

“nia ya mkuu wa Wilaya hapa na mimi ni kuhakikisha kazi zote zinafanywa na watu wa Kidabaga ili hela yote izunguke hapa hapa Kidabaga na sio watu kutoka nje, hivyo atakuja afisa maendeleo kuwapa mafunzo katika vikundi ili mfanye hizo kazi vizuri”

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.