WCB KWACHAFUKWA

Unakumbuka ile big ishu ambayo ilitrend kwa kitambo fulani kufikia hatua kumpeleka Nandi mahakani?. Naongelea Ishu ambayo ilihusisha kuvuja kwa video ambayo ilitafsiriwa kuvunja maadili ya kitanzania kwa kusambaza mambo ya faragha hadharani. Video hiyo ilikuwa ikimuonyesha Nandi na msanii mwenzake Bilnas katika mazingira tatanishi ya kimahaba chumbani.

Moja kati ya mambo mengi na fikra nyingi kutoka kwa fans wa industry ya entertainment ni kwamba waliamini Nandi alifanya hivo kwa ajili ya kiki japo alikanusha ya kwamba hakuwa akifahamu chochote juu ya chanzo cha kuvujisha video hiyo.

Time zimekwenda na ishu ikionekana kwamba imekwishapotea masikioni pa watu huku Nandi akiendelea na mishemishe zake stori kwa sasa iko hivi:

Kwanza kabisa video ya Nandi na Bilnas ilianzia kwa jamaa mmoja anayemiliki blog ya Udakutz  ambaye ndiye alianza kusambnaza video hiyo ya Nandi na Bilnas Faragha.

Siri imefichuka ikielezwa kutoka kituo cha polisi kati kupitia kanda maalumu Dar es salaam (central) kwamba mameneja wa Diamond platnumz na team WCB Babu tale na mwenzake Sallam Sk pamoja na mmiliki huyo wa blog ya Udakutz ambaye alivujisha video hiyo kupitia IG account yake wanatafutwa na polisi mahali popote walipo wakamatwe kwani wanashitakiwa kuhusiana na wao kuwa ndio wahusika wakuu wa kuvuja kwa video hiyo.

Taarifa ya polisi inasema kwamba watu hao watajwa hapo juu wanahitajika kwenda kujibu tuhuma za uhalifu wa kusambaza video ya udhalilishaji kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.Taarifa hizi zimetoka kwenye IG account ya Soud Brown wa Clouds media ambaye alipost taarifa hiyo.

Kuhusiana na mmiliki wa blog na page ya Udakutz inasemekana kwamba yupo chini ya ulinzi wa polisi kufuatia kukamatwa na kuhojiwa kwa masaa kadhaa ambapo bwana Udaku aliwataja watuhumiwa hao wawili kuhusika katika kumpenyezea video ya udhalilishaji  dhidi ya msanii Nandi pamoja na Bilnas.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.