Waziri Mwakyembe amteua Leodger Tenga kuwa Mwenyekiti BMT

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amemteua Leodger Chilla Tenga kuwa mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kuwateua wajumbe sita wa baraza hilo.

Uteuzi wa Wajumbe hao sita ambao ni, Mkumba Mtambo, Beatrice Singano, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa, Joseph Ndumbaro, Salmin Kaniki na Rehema Madenge, umeanza rasmi jana Februari 8, 2018.

Vile vile, ameteua wajumbe wengine watatu wa BMT kutokana na nafasi za vyeo vyao, akiwemo Yussuph Singo aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Na Edicome Shirima kuwa Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya Ufundi, pamoja na Mohammed Kiganja aliyemteua kuwa Katibu Mkuu wa BMT.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.