WAZIRI MKUU WA PAKISTAN ATOA AMRI YA KUBOMOLEWA NYUMBA YA GAVANA WA PUNJAB

Punjab, PAKISTAN.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan, hivi majuzi alitoa amri ya kubomolewa kuta za nyumba ya Gavana wa jimbo la Punjab, iliyoko katika mji wa Lahore, katika mwendelezo wa ahadi yake ya kuzigueza nyumba za Waziri Mkuu na Magavana kuwa maeneo ya wazi kwa ajili ya wananchi.

Katika mwendelezo wa kampeni yake hiyo, ambayo ni ya kupambana na mambo ya kifahari na kuondoa ufa wa kitabaka baina ya wananchi na wanasiasa wa Pakistan, Bw Khan ametoa amri ya kubomolewa kuta zilizozunguka nyumba ya gavana wa jimbo la Punjab katika mji wa Lahore na kuligeuza jengo hilo kuwa eneo la matumizi ya umma.

Waziri wa Habari na Utamaduni wa jimbo la Punjab, Fayyazul Hassan Chohan, amethibitisha kutolewa amri hiyo na Waziri Mkuu Khan na kueleza kwamba kazi hiyo ya ubomoaji wa kuta za jengo hilo itakamilika katika muda wa siku mbili hadi tatu.

Aidha, Waziri wa Elimu wa Punjab, Shfqat Mehmood, alieleza hapo awali kwamba, jengo la ofisi ya gavana wa Punjab litageuzwa makumbusho na ukumbi wa sanaa, huku eneo lake la nje litafanywa bustani ya umma itakayokuwa na bustani ndogo pia ya wanyama.

Kiongozi hiyo na mtendaji mkuu wa Pakistan amesisitiza pia kwamba, karibuni hivi hatua sawa na hiyo itachukuliwa katika miji ya Peshawar na Karachi ambapo wananchi wataweza kutumia bustani zitakazojengwa kando ya majengo hayo ya kifahari ya serikali.

Kabla ya uchaguzi wa bunge la Pakistan, Bw Imran Khan alitoa ahadi ya kuondoa ufa wa kitabaka uliopo kati ya raia na viongozi wa serikali na kushajiisha wanasiasa wa Pakistan wazoee kuishi maisha ya kawaida.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.