WAZIRI KIGWANGALLA NA WAKILI KARUME WAWEKA HISTORIA

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangalla amekutana na kufanya kikao chake cha chakula cha mchana na Wakili Fatuma Karume kujadili jinsi ya kuboresha uhusiano baina ya viongozi wanapowasiliana kutumia mitandao ya jamii na kuwa mfano bora kwa vijana wanaochipukia kwenye uongozi.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Waziri Kigwangalla ameandika kuwa, “ Tuache utani pembeni, Siasa pembeni. Kuna la kujifunza katika hadithi hii; Shangazi ni mtu poa sana, mnyenyekevu, mvumilivu, msikivu, mwenye uelewa mpana wa mambo, na anasababu zake katika kila anachokifanya.

Aidha Kigwangalla amesema, mkutano huo unatoa funzo kwa watu wote kuvumiliana, kuelewana, kuwa na huruma sambamba na kuwa wamoja na kuheshimiana, huku akihimiza kila mmoja kuendelea kuboresha kilicho mbele yake.

Itakumbukwa wawili hao mwaka jana, waliingia katika malumbano makali na kufikia kutoleana maneno mabaya na yenye lugha za matusi tukio lililopokelewa kwa hisia tofauti

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.