WAZIRI KIGWANGALLA KUPASUA JIPU ASUBUHI HII

Na Wilson Pastory.

Dodoma. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla leo Alhamisi Januari 25, 2018 anatarajia kuzungumza na wanahabari mjini Dodoma kuanzia majira ya saa 4 Asubuhi.

Kupitia taarifa aliyoitoa jana usiku kwenye ukurasa wake wa twitter, Mhe. Kigwangalla amesema Mkutano huo na wanahabari utafanyika kwenye ukumbi wa Swagaswaga house.

Amesema atazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu wizara ya Maliasili na Utalii, huku akitarajia kuweka hadharani orodha ya watuhumiwa mbalimbali wa ujangili hapa nchini.

Taarifa ya Mhe. Kingwangalla kama alivyoandika kwenye ukurasa wake wa twitter

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.