WAZIRI KAIRUKI AZITAKA KAMPUNI ZA MADINI KUTAFUTA SULUHU AMA KUKUBALI KUFUNGIWA

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amezitaka kampuni za Mundarara na Sendeu Mining zinazofanya shughuli za uchimbaji wa Madini ya Ruby kukaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro wao na endapo itashindikana basi Serikali itachukua hatua za kuufungia mgodi huo.

Agizo hilo amelitoa mapema leo alipotembela katika kijiji cha Mundarara Wilaya ya longido Mkoani Arusha kufuatia mgororo uliopo katika eneo hilo kutokana na muingiliano wa chini ya ardhi baina ya kampuni mbili za Mundarara na Sendeu Mining, zinazofanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo, hali iliyosababisha mzozo mkubwa baina ya kampuni hizo.

Aidha amesema mgogoro huo wa chini ya ardhi ambao kwa kitaalamu unaitwa ‘Mtobozano’, umesababisha taharuki kubwa kufuatia kuripotiwa kwa matukio kadhaa ya kutishiana silaha za moto baina ya kampuni hizo mbili zinazofanya shughuli zake katika eneo hilo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.