WATU KUMI NA MBILI WAUAWA KWENYE MACHAFUKO MAPYA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Bria, AFRIKA YA KATI.

Miili ya watu kumi na mbili, pamoja na miili ya wanawake kumi, imegunduliwa siku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa asubuhi huko Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo inasemekana waliuawa na kundi la zamani la waasi la Seleka kwa kulipiza kisasi shambulio dhidi ya moja ya misafara yao.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka nchini humo vilivyohojiwa na VOA Afrique, watu hawa waliuawa katika Shambulio ambalo linadaiwa kuwa lilitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Wakikristo la Anti-balaka kilomita 7 kutoka katika mji wa Bria kwenye barabara inayoelekea Ippy.

Vyanzo hivyo vinasema kwamba watu waliouawa wengi wao walikuaa wakimbizi wa ndani kutoka kambi ya PK3, iliyo karibu na kambi ya jeshi la Umoja wa Mataifa nchini humo (Minusca).

Kutokakana na mauaji hayo, watu kadhaa walikimbia makazi yao, na hapo jana wameandamana mbele ya kambi ya Minusca wakionyesha uzembe wa kikosi hiki cha Umoja wa Mataifa.

Polisi iliingilia kati na kutawanya waandamanaji hao kwa kutumia gesi za machozi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.