WATU 16 WANAODAIWA KUWA NI WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA ILALA

 

Naibu Kamishna uhamiaji, Afisa uhamiaji Ilala Pili Zuberi Mdanku kwa kushirikiana na OCD Ilala SP Jason Ibrahim wamefanikiwa kuwakamata watu 16 wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu katika kata ya Mchikichini Jimbo la ilala.

Hatua hiyo, imekuja mara baada ya mmoja wa wananchi kutoa kero kwa mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuwa kuna nyumba ambayo inawahifadhi wahamiaji haramu.

DCI Pili ameamua kufanya doria katika eneo hilo mara baada ya kupata taarifa hizo kwani, si mara ya kwanza kufanya doria katika eneo hilo na kuwakamata wahamiaji haramu.

Amesema kuwa, katika mahojiano ya awali walioyafanya na wahamiaji hao, wamedai kuwa  watu 15  wana  asili ya Kigoma na mmoja ni msambaa, ambapo wamechukuliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kwa upande wake, DC Mjema amewapongeza Afisa uhamiaji Ilala na timu nzima ya OCD kwa kufanya kazi kubwa ya kuwafichua watu hao wanaodhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu.

Amesema kuwa, nchi ya Tanzania haimkatazi mtu kuishi nchini humo, bali itamtaka kila mtu kufuata sheria,taratibu na kanuni za kuishi nchini humo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.