WASIKIE CCM KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole ameweka wazi mipango ya chama hicho katika kujiandaa na Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kumbainisha mgombea kiti cha urais 2020 kupitia chama chao.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole
Polepole kupitia mahojiano yaliyofanyika leo Jan 09 katika kipindi
cha East Africa BreakFast amesema kuwa alichokifanya Rais Magufuli kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani, ni dhahiri kuwa hakuna mwingine atakayepewa ridhaa na chama zaidi yake kugombea 2020.

“Mwaka 2020 hatuna shaka katika nafasi ya Urais mgombea wetu ni Rais Magufuli hatuna wasiwasi kabisa na kiongozi wetu kwa aliyofanya kwa kipindi hiki njia ni nyeupe, lakini hatujakataza wengine kuchukua fomu wao wachukue tu“, amesema Polepole.

Akizungumzia kupunguzwa kwa wanachama wanaotakiwa kupiga kura za maoni amesema kuwa, “Sisi hatuukatai ubaya ambao ulikuwepo zamani, tunakiri na kufuta kwa kufanya mema, CCM tuna kadi za kielektroniki hivyo huwezi kupiga kura ya maoni, kama huna kadi ile na sio kwamba tumewapunguza bali ni mabadiliko ya teknolojia hivyo wahakikishe wanakubaliana na mabadiliko na hakuna aliyefukuzwa“.

Aidha Polepole amesema kuwa chama chake, hakipokei tena watu wanaotoka upinzani wao wabaki hukohuko usajili umeshafungwa, na kudai kuwa waliobaki hawana vigezo na wajiandae kuachia majimbo 2020.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.