Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linalaani vikali tukio linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandiishi wa habari wa Wapo Redio Sillas Mbise lililotokea Tarehe 08.08.2018 siku ya mechi kati ya Simba vs Asante Kotoko ya nchini Ghana, ikiwa ni maadhimisho ya Simba day.
Aidha Polisi kanda maalum imeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha ya video hiyo inayosambaa inayoonesha askari wa Polisi na mwandishi huyo wa habari ili kubaini ukweli.
Sambamba na hayo Polisi jukumu lake kuu ni kulinda usalama wa raia na mali zao na si kuwapiga raia walitenda kosa ambao hawajakataa kutii sheria ya kukamatwa.