WALIMU NA VIONGOZI WA KIJIJI WATAKIWA KUPUNGUZA UTORO MASHULENI

Longido

Mbunge wa Jimbo la Longido Mhe Dr Steven Kiruswa ameendelea na ziara leo ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika jimbo hilo.

Katika ziara hiyo, amekagua ujenzi wa tenki kubwa la maji unaondelea katika kata ya Gilai-Meirungoi na kuona namna ujenzi unavyoendelea.

Mbunge alitembelea ujenzi wa shule mpya ya msingi ya kijiji cha Meirugoi kata ya Glai-Meirugoi unaondelea na kushirikiana na Mafundi kupanga mawe.

Aidha amewahimiza viongozi wa kijiji cha Magadini pamoja na walimu wa shule ya msingi Magadini kutengeneza mkakati bora ili kupunguza utoro shuleni, na pia wahakikishe wanafunzi wanapata chakula.

Aidha amewakumbusha, wananchi pamoja na viongozi wao juu ya kuchangia mfuko wa elimu ulioanzishwa na mbunge huyo ili uweze kusaidia walimu katika majukumu yao.

Katika ziara hiyo, mbunge Kiruswa alikua ameambatana na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na afisa elimu wa shule ya msingi, viongozi wa idara ya elimu wilaya, afisa tarafa ndugu Lee pamoja na mtaalamu wa maji ambapo wameweza kuwasikiliza wananchi na kutatua changamoto mbalimbali.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.