WAKO WAPI YANGA WALE WA KUTOFUNGWA?,WANALAMBALAMBA WAWALAMBISHA MAGOLI 3.

 

NA KAROLI VINSENT.

MAJANGA kwa mabingwa wa kihistoria timu ya Soka ya Yanga baada ya kuchapangwa bila huruma ni timu ya wanalambalamba ya Azam Fc kwa mabao 3 kwa nunge kwenye michuano ya mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.

Yanga ambao kwa sasa wanarekodi ya kipekee kwenye ligi kuu soka ya Tanzania Bara baada kucheza mechi 18 bila kufungwa huku mchezo wao wa mwisho wakibakisha na wanalambalamba hao wamalize mzunguko wa kwanza wa ligu kuu.

Muuaji mkubwa kwenye mtanange huo wa kusisimua alikuwa Obrey Chirwa alifunga mabao mawili dakika ya 33 akipokea pasi kutoka kwa Tafadzwa Kutinyu na dakika ya 60 kipindi cha pili alifunga bao la tatu.

Ennock Atta alifunga bao la pili dakika ya ya 44 kwa mpira wa faulo akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto uliozama moja kwa moja langoni na kumaliza Karama ya mabao katika mechi hiyo.

Baada ya mechi hiyo msimamo umekuwa hivi kuwa Azam anaongoza kundi B akifuatiwa na Malindi wote wakiwa na Pointi nne, Yanga anashika nafasi ya tatu akiwa na pointi tatu, KVZ nafasi ya nne akiwa na pointi nne tatu nafasi ya tano inashikwa na Malindi ikiwa na pointi moja.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.