WAJUMBE WAPYA KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA WAAPISHWA.

Zanzibar, Mjini.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, jana amewaapisha wajumbe wapya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar.

Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Washauri wa Rais, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji.

Wajumbe walioapishwa katika hafla hiyo ni Dk. Mohamed Seif Khatib, Mbaraka Mohammed Abdulwakil na Sheikh Hassan Othman Ngwali.

Wengineo ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mohammed Mussa Wadi, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wa Serikali.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.