WAJASIRIAMALI NA WATAALAM WA TIBA NA DAWA BARIDI KANDA YA ZIWA WAKUTANA NYAMAGANA MWANZA.

Mwanza

Na mwandishi wetu,

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, leo October 19 wamekutana Wilani Nyamagana katika semina elekezi ya kuwajengea uwezo watoa huduma na wamiliki wa maduka ya dawa baridi.

Katika taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya mbunge wa jimbo la Nyamagana imeeleza kuwa, Mkuu wa mkoa Mwanza pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza yawakutanisha wajasirimali, wataalumu wa Tiba na Dawa”Pharmacist” 800 kutokea mikoa ya Kanda ya Ziwa katika semina elekezi kwa siku tatu kwanzia 15-19/10/2018 Wilayani Nyamagana.

Imeeleza kuwa, Semina hiyo elekezi ni mkakati wa Wizara katika mpango wake kabambe kuwajengea uwezo watoa huduma na wamiliki wa Maduka ya Dawa baridi kibiashara kupitia mafunzo ya ujasirimali, uchambuzi wa sheria, taratibu pamoja na kanuni mbali mbali za uendeshaji wa biashara.

Mafunzo hayo kwa Kanda ya Ziwa yameendeshwa na Mkufunzi George Marwa pamoja na Tibaijuka kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ndg. Antoni Yesaya kutokea Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza pamoja na Ndg. Halidi Mashashi kutokea Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.