WAFANYABIASHARA WANAOKWEPA KODI WAPEWA SOMO KAGERA

Na Allawi Kaboyo-Bukoba Kagera.

Mkuu wa mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wafanyabiashara mkoani humo kuacha tabia ya kufunga maduka yao palea wanapowaona maafisa wa TRA wakija katika maduka yao na kumuagiza meneja TRA wa mkoa huo kujenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara pamoja na kutoa elimu ya kutosha ya umuhimu wa kulipa kodi.

Mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo katika kikao chake na wadau wa kodi,maafisa wa TRA pamoja na wafanyabiashara kilichofanyika january 11 mwaka huu kwenye ukumbi wa manispaa ya Bukoba kikiwa na lengo la kujua hali ya ulipaji kodi mkoani Kagera na mwelekeo wa mkoa katika suala zima la kulipa kodi.

Gaguti baada ya kusikiliza maoni ya wafanyabiashara amewaagiza maafasa wa mamlaka ya mapato TRA kuacha kuwavizia wafanyabiashara na badala yake wawafate na kuwaelimisha ili kuweza kupata urahisi wa ukusanyaji wa mapato.

“Ni lazima TRA kutengeneza mahusiano mazuri na wafanyabiashara, hakuna sababu ya mfanyabiashara kumuona afsa wa TRA kisha kufunga biashara yake na kukimbia duka, niagize kuanzia leo sitaki kusikia wala kuona hali hii inaendelea katika mkoa wa kagera. Wafanyabiashara lazima wawe hulu katika nchi yao lakini pia na nyie TRA acheni kuwavizia waiteni na ikiwezekana wafateni wape elimu ya kutosha na mwisho wa siku kodi watalipa bila kusumbuana.” Amesema Gaguti.

Kwaupande wake katibu tawala mkoa wa Kagera prf.FAUSTINE KAMUZORA akiongea katika kikao hicho akawataka wafanyabiashara hao kuwa na imanai na serikali ya awamu ya tano katika suala zima la ulipaji kodi kwamba haupo kwaajili ya kumkomoa mtanzania au mfanyabiashara yeyote na kuahidi kuwashughulikia watendaji watakaowakwamisha wafanyabiashara hao suala lililompelekea kutoa namba yake ya simu ya mkononi.

Badhi ya wafanyabiashara hao wakieleza changamoto wanazokumbana nazo kwenye biashara zao wamesema kuwa TRA imekuwa ikifanya kazi ya ya kuwavizia katika biashara zao na muda mwingine kufikia uamuzi wa kuwafungia maduka yao pasipokuwapa elimu ya mlipa kodi.

Aidha wafanyabiashara hao wameongeza kuwa suala la kukadiriwa kodi halifanyiki kwa usawa na haki kama inavyostahili na suala linalowapelekea wafanyabiashara wengine kuanza kuhama na kwenda nje ya nchi.

Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho mkuu wa mkoa amefanya ziara ya kushutukiza katika maeneo mbalimbali ya maduka katika mji wa Bukoba pamoja na soko kuu la mji mji huo ambapo akiwa huko ameweza kuongea na wafanyabiashara hao juu ya mwenendo wa biashara zao na kuaahidi kuztatua kero zinazowasumbua katika kuendesha biashara zao za kila siku ambapo pia amewasisitiza kulipa kodi kwa wakati na kusisitiza matumizi sahihi ya mashine za EFD’s.

MWISHO:

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.