UGANDA POLISI WATUMIA MABOMU KUWATAWANYA WAANDAMANAJI WA KUPINGA KODI YA MITANDAO YA KIJAMII

KAMPALA. Nchini Uganda Jeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi leo kuwatawanya mamia ya waandamanaji katika mitaa mbalimbali, ambao walikuwa wanapinga tozo jipya la kodi kwa matumizi ya mitandao ya kijamii.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa polisi pia walijaribu kumkamata kiongozi wa maandamano hayo Mwimbaji Robert Kyagulanyi, ambaye pia hujulikana kama “Bobi Wine”, Mbunge wa jimbo la Kyaddondo Mashariki kutoka wilaya ya Wakisso Mkoa Kati nchini humo lakini alifanikiwa kukimbia.

Kodi hiyo iliyoanza kukatwa mwanzoni mwa mwezi huu, inamlazimu mtumiaji wa mitandao kama Facebook, WhatsApp Twitter na hata Instagram kulipa Shilingi 200 za Uganda($ 0.05, £ 0.04, Tshs 116, Kshs 5) kwa siku moja kabla ya kutumia huduma za mitandao hiyo.

Bunge la Uganda lilipitisha kodi hii hapo Mei baada ya Rais Yoweri Museveni kusukumwa na mabadiliko, akisema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ikichangia sana kusambaza habari za zisizo za kweli(uvumi), Lakini wengine wanasema kwamba ni njia ya kuzuia maoni muhimu kuhusu serikali.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.