VYUO VIKUU NCHINI KUZALISHA VIJANA IMARA WATAKAOWEZA KUSHINDANA KATIKA SOKO LA AJIRA

 

 

Serikali imevitaka Vyuo Vikuu nchini, kutengeneza Vijana wenye uwezo mkubwa watakao ingia kwenye soko la ajira kwa nchi za Africa na kote Ulimwenguni bila kikwazo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa Uliokutanisha Vijana ambao biashara zao ziko kwenye hatua za awali na ambao wanatafuta marafiki wa biashara, unafahamika kama Innovation in the Data Age.

Ikupa amesema Africa kwa sasa inakadiriwa kuwa na watu bilioni moja nukta mbili, hivyo kunafursa ya uwepo wa ajira na fursa za biashara na kwamba Ripoti ya Banki ya Dunia, inaonyesha Vijana Milioni moja tu kwa mwaka nchini Tanzania wanaoingia katika ajira.

Amesema ipo haja ya Vyuo hivyo kuweka mifumo itakayowapa uwezo na ujasiri wa kupenya popote Africa kutafuta fursa za biashara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Venture ambaye ni Mratibu wa Mkutano Jumanne Mtambalike amesema mkutano huo utafungua mwanya wa kujadili sera na sheria za nchi namna ambavyo zinawezwa kuboreshwa na zikawa na mazingira mazuri ya kuwasaidia vijana na Wafanyabiashara wadogo kufanya biashara kwa uhuru.

Naye Katibu Mtendaji Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi, Being’i Issa amewataka Vijana kutumia mitandoa ya kijamii katika kutangaza biashara zao.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.