VURUGU ZATANDA UKANDA WA GAZA, WAPALESTINA ZAIDI YA THERASINI WAJERUHIWA

Vurugu zimeendelea huko katika Ukanda wa gaza na ukingo wa Magharibi ambapo zaidi ya Wapalestina thelathini wamejeruhiwa katika makabiliano na Polisi wa Israel.

Matukio haya ya vurugu yamekuja kufuatia Rais Donald Trump kutangaza kuutambua mji wa Yerusalemu kuwa Mji Mkuu wa Israel.

Tangu rais Trump alipotangaza rasmi kuutambua mji huo wa Jerusalem, Wapalestina  wameonekana kutokukubaliana na maazunguzi hayo ya rais huyo wa Marekani na hivyo kufanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuchoma picha za rais huyo wa Marekani.

Wakati huo huo Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na Makamu wa Rais Marekani, Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu.

Waandamanaji wamechoma matairi na kurusha mawe huku maafisa usalama wa Israel wakifyatulia wandamanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira.

Huko katika Ukanda wa Gaza, kundi la kiislamu la Hamas limeitisha intifada au mapambano ambapo Omary Shakir Mkuu wa Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch katika eneo la Isreal na Palestina yupo mjini Ramala.

Shakir ameiambia BBC kuwepo baada ya Israel katika eneo hilo kwa miongo kadhaa sasa wapelestina wengi wamekuwa na hasira na tangazo la Rais Trump.

Kwa upande wake Naibu Waziri anayehusika na masuala ya Diplomasia wa Israel Michael Oren ameimbia BBC kuwa tangazo la Rais Trump limeleifanya iwe siku ya furaha kwa kwa taifa la Israel ameseema mamlaka ya Israel ilitarajia vurugu kutoka kwa wapalestina.

Vurugu zaidi zinatarajia kuendelea hii leo huku kikao cha dharala cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kikiendelea.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.