UWT WILAYA YA UBUNGO YAAHIDI KUREJESHA JIMBO 2020.

Dar es salaam.

Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ubungo, wameahidi kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 Chama cha Mapinduzi (CCM) kitashika dola katika jimbo la Ubungo na kurejesha kata zilizopotea ambazo kwa sasa zinakaliwa na wapinzani.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa umoja wa Wanawake mkoa wa Dar es Salaam, Doroth Kilave, wakati wa maadhimisho ya wiki ya wanawake wa chama hicho.

“Wanawake wa UWT ni jeshi kubwa kwa umoja wetu tutahakikisha tunalinda dola, chama kinashinda chaguzi zake katika jimbo la Ubungo na majimbo mengine yaliopo katika mkoa huu”amesema Kilave.

Kilave amesema, lengo la CCM ni kushika dola, ambapo amezitaka jumuiya kushirikiana na kila mmoja anashika majukumu yake UWT ipo mstari wa mbele katika kusimamia chama, aidha amewataka wanawake wa Wiĺaya hiyo kuungana katika chaguzi za mtaa wachukue fomu wagombee wakikosa wagombea udiwani katika kata zao na Ubunge

Amesema kuwa, katika wiki ya wanawake wa CCM wilaya hiyo, UWT waliadhimisha kwa makongamano pamoja na kutembelea kambi ya watoto yatima Mburahati na kukabidhi misaada ya vyakula na kufurahi na watoto wa kambi hiyo.

Kwa upande wake Katibu wa UWT wilaya hiyo,Sophia Kiwanga amesema wilaya hiyo imekuwa miongoni mwa wilaya tano zinazounda mkoa wa Dar es saalam zimegawanyika katika tarafa mbili za Magomeni na Kibamba.

Sophia amesema wilaya hiyo ina wakazi 1,031,349 kichama ina kata 14 matawi 137 idadi ya wanawake wam UWT 28,000, mpango mkakati kuelekea chaguzi za serikari ya mtaa UWT imeweka mkakati madhubuti kuelekea chaguzi hizo mwaka 2019.OK

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.