UWEKEZAJI BILA SIASA UNAWEZEKANA :ISSA SAMMA

Na Mwandishi wetu -NGARA KAGERA


Msemaji wa wawekezaji kutoka Korea Kusini katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera Issa Samma amesema wakazi wa wilaya hiyo na viongozi wao wanaweza kukubali au kukataa uwekezaji bila kulumbana kwa kutanguliza siasa, ukanda na ukabila.

Samma ametoa kauli hiyo siku chache baada ya mbunge wa jimbo la Ngara Alex Gashaza kunusurika kupigwa na wananchi wa kijiji cha Kazingati akipinga utaratibu uliotumika wa kuwagawia ardhi wawekezaji wa Korea Kusini wilayani Ngara.

Amesema wawekezaji walijitokeza kutaka ardhi ya kilimo na kujenga viwanda Kuanza katika kijiji cha Kazingati kata ya keza wilayani Ngara wakilenga kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kufundisha teknolojia ya kilimo na viwanda kuharakisha maendeleo.

“Pamoja na kwamba sikupaswa kusema lolote lakini mimi ni Mbia katika uwekezaji , kwanza Nawapongeza wote wanaotaka kujua ukweli pia Nampongeza Mbunge Gashaza kwa kufatilia na kufika kwenye Mradi unapotegemewa” Alisema Samma

Alisema Wakorea hawajapewa ardhi inayotajwa kuwa ni ekari 12,000 Isipokuwa Halmashauri Ilisaini MOU kwa kuonyesha utayari wa Ardhi kuwepo Ekari 12000 walizohitaji kwa maana nyingine mchumba yupo aitwaye ardhi wilayani Ngara.

Pia alidai Halmashauri iliomba kila kijiji yaani vijiji 72 vyote vya wilaya ya ngara Ekari 1000 kwa muwekezaji na barua hizo zipo vjiji vyote vya wilaya Kikiwemo na kjiji cha kazingati ambacho kilichoonyesha kuwa tayari Kutoa Ekari 50 kisheria na mahiyaji ya ziada yangeshughulikiwa na TIC

Kwa mujibu wa Sheria za iwekezaji Ardhi ya kijiji inayotolewa ni Ekari 50 wilaya Ekari 100 baadaye Wilaya inaomba kwa kamishina wa Ardhi kwa niaba ya Rais, hata hivyo hii ni kwa Mtanzania Si kwa mgeni ambaye anaombewa na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC)

Kuhusu Ekari 8000 zinazozungumziwa , alisema zipo kitongoji cha Muko Gwenzaza na 4000 kitongoji cha Misalasi (Free land) hazina wakazi Isipokua Wafugaji Wachache..hizo Ndizo muwekezaji alionyeshwa, akahiali kuwekeza ngara viwanda viwili vya kahawa na mbolea na kuendesha kilimo

“Kama muwakilishi a Mkorea wilayani Ngara, Sitakubali mwananchi adhulumiwe ardhi yoyote ile , kama kuna uhalibifu wa mazingira Sheria ipo km Ilivyotumika kwa wakimbizi Benaco Ili kurudisha uoto hivyo uwekezaji huu ni juu yetu kuukubali au kuukataa” Alisema

Mbunge wa jimbo la Ngara Alex Gashaza juzi alikwenda katika kijiji cha kazingati kuwaelimisha kuwa mwekezaji kutoka Korea kusini alipata ardhi kijijini humo bila kufuata taratibu na hakuna mikutano ya hadhara wala baraza la madiwani kupitisha ardhi kutwaliwa

Kauli ya mbunge huyo ilimpatia wakati mgumu na kushondwa kumaliza mkutano wake akizomewa huku watu wakitawanyika naye kuomba ulinzi kwa jeshi la polis ambalo askari wa jeshi hilo walitanda mkutanoni baada ya kuwepo tetesi za vurugu kutokea.

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Aidan Bahama amewataka wananchi kuvumilia wakati mchakato huu wa uwekezaji ukifanyiwa kazi na serikali kuu ili hatimaye mhisika aruhusiwe kisheria na kuwekeza miradi ya kiuchumi kwenye maeneo yao.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.