UTAFITI WA IEP:UBAGUZI WA RANGI UMEONGEZEKA DUNIANI.

 

Sydney, AUSTRALIA

Taasisi moja binafsi inayoshughulika na masuala ya Uchumi na Amani (IEP) duniani, imeeleza kuwa, katika ripoti yake mpya ya mwaka huu 2018, vitendo vya ubaguzi wa rangi viliongezeka na takwimu za watu waliouawa kutokana na mashambulio ya kigaidi zimepungua katika mwaka uliopita wa 2017.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na taasisi (IEP) hiyo ya Institute for Economic and Peace yenye makao yake mjini Sydney, Australia, vielezo vya kimataifa kuhusu ugaidi katika mwaka 2018 vinaonyesha kuwa, maafa ya roho za watu yaliyotokana na mashambulio ya kigaidi katika mwaka 2017 yalipungua kwa asilimia 27, lakini kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) lingali ni kundi hatari zaidi la kigaidi duniani.

Katika mwaka huo uliopita (2017), nchi 67 zilishuhudia kwa ukaribu kesi moja ya mtu aliyeuawa kutokana na shambulio la kigaidi, kiwango (cha idadi za nchi) ambacho ni cha chini kulinganisha na mwaka 2016, ambapo wakati katika mwaka 2016 nchi 79 ziliripoti tukio lisilopungua moja la kifo kilichotokana na hujuma ya kigaidi.

Sehemu nyingine ya ripoti ya IEP imeeleza kuwa, nchi za Afghanistan, Nigeria, Somalia, Pakistan, Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na India, ni miongoni mwa nchi zilizoripoti idadi kubwa zaidi ya vifo vilivyosababishwa na mashambulio ya kigaidi.

Ripoti hiyo ya IEP kwa ajili ya Uchumi na Amani, imebainisha pia kuwa watu 17 waliuawa katika jumla ya hujuma na mashambulio 31 yaliyofanywa na makundi ya mrengo wa kulia yenye misimo mikali na chuki za ubaguzi wa rangi, ambapo mengi ya mashambulio hayo yalifanywa na mtu mmoja mmoja dhidi ya Waislamu.

Kwa mujibu wa IEP, jinai na uhalifu uliofanywa na makundi hayo ya mrengo wa kulia yenye misimamo ya kufuturu mpaka viliongezeka katika nchi za Marekani na Canada, ambapo mnamo mwezi uliopita wa Novemba, Polisi ya Upelelezi ya Marekani (FBI), ilitangaza kuwa uhalifu uliofanywa kutokana na chuki umeongezeka kwa asilimia 17 mwaka huu kulinganisha na 2017, wakati nchini Canada ongezeko hilo ni la karibu asilimia 50.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.