UPINZANI BADO HALI TETE, MWINGINE ATIMKIA CCM

Na Danson Kaijage,Chamwino

LICHA ya wadau mbalimbali pamoja na viongozi wa Dini kukerwa na hamahama ya wanasiasa kutoka chama kimoja na kuingia chengine na kusababisha kurudiwa kwa uchaguzi mdogo bado mchezo huo unaendelea.

Hali hiyo imetokea juzu baada ya aliyekuwa Diwani wa Chadema kata ya Chinugulu wilaya ya Chamwino, Amosi Henely Fumaa kuondoka Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Diwani huyo ambaye pia alikuwa wa Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mtera, ametangaza kujiuzulu nafasi zote kwa madai kuunga mkono kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari, Fumaa amesema kuwa, ameamua kuhamia CCM kwa hiari yake kutokana na harakati zinazofanywa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kuwatetea wanyonge na kuwaleta maendeleo ya kweli katika kila ngazi.

”Tarehe ya leo 13, Septemba nimeamua kuhama Chadema na Kujiunga na CCM kwa sababu Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dkt.Magufuli inafanya kazi nzuri na kila mpenda maendeleo anaona hivyo sioni sababu ya kulumbana na Serikali iliyopo Madarakani kwani Upinzani hauna dira ya maendeleo kwa wananchi”amesema Fumaa.

Pamoja na kuwepo kwa kauli kuwa wanaohama Chadema wananunuliwa Fumaa alisema kuwa hakuna Diwani yoyote yule anayenunuliwa na CCM bali ameamua kurudi CCM kutokana na Serikali kufanya kazi nzuri na kuwasihi wanadodoma kuhakikisha wanaichagua CCM inayotekeleza Ilani ya Chama na wananchi kupata maendeleo.

”Kwangu ni Uzalendo kwanza hata kama ni adui yako unapomuona anafanya mambo mema kwa jamii huwa na muunga mkono hivyo nitashirikiana na Chama changu hiki na kuwaletea maendeleo wananchi kwani Chadema nilipotea tu” amesema Fumaa.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chamwino, Francis Gombo, amesema kuwa Chadema watapata tabu sana hivyo anmkaribisha, Amosi Henely Fumaa kwenye chama kinachotekeleza Ilani ya Chama kwa wananchi wote na kila mtu anaona maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Rais wetu Dk.Magufuli.

”Tunajua Chadema ulikuwa unapita njia tu hivyo tunakuambia karibu nyumbani na tuendelee kumunga mkono Rais wetu ili aendelee kutupatia maendeleo bora”alisema Gombo

Hata hivyo Gombo Hata hivyo Gombo amesisitiza kuwa hakuna Diwani yoyote anayenunuliwa na CCM, bali wanarudi CCM kutokana na Serikali kufanya kazi nzuri na kuwasihi wananchi waendelee kuwa na imani na CCM ambayo ni mkombozi wa wanyonge na kuhakikisha wanaichagua CCM inayotekeleza ilani ya chama kwa maendeleo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.