UPEPO MKALI NA MAWIMBI YAVIKUMBA VIJIJI VYA THAILAND.

 

Na. Jovine Sosthenes

Mvua, upepo mkali na mawimbi vimelikumba eneo la kusini mwa Thailand hususani katika maeneo ya vijiji vilivyo jirani na fukwe ikiwemo maeneo ya utalii yaliyokumbwa na kimbunga kikali cha Papuk.

Hakuna taarifa ya vifo lakini tayari mamlaka ya hali ya hewa nchini humo imetoa tahadhari huku ikishuhudiwa mamia ya watalii wakiondoka katika maeneo waliyokuwepo.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imesema kimbunga kingine kikubwa kinatarajiwa kupiga jioni ya leo na kitakua kina kasi ya kilomita 80 kwa saa.
Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga zaidi eneo la Nakhon na kuleta mvua kubwa na upepo mkali katika maelfu ya vijijini.

Mamlaka nchini humo imewataka wakazi wa eneo hilo kuondoka mara moja kutokana na hali hiyo huku kabla barabara hazijafungwa.
“Hapana huwezi kukaa hapa, kila kitu kitachukuliwa hapa na kila mwaka maeneo ya hoteli huharibiwa lakini kwa wakati huu tuna kimbunga kikubwa kinakuja hakuna kitakachobakia”
Maafisa wengine wameonekana maeneo ya Pwani wakiwasaidia wavuvi kuondoa boti zao zisije kuchukuliwa na mawimbi.

Mapema jana Waziri mkuu wa Thai, Prayuth Chan-Ocha alionekana akiwa na magavana wa maeneo hayo wakitoa tahadhari za kuchukuliwa na vifaa vya matibabu na dawa.

Hata hivyo mamlaka nchini humo imezuia huduma za usafiri wa majini na kuanza kuokoa nyingine zinazopelekwa na maji.

Kimbunga hicho kinahofiwa kuwa kikubwa kutokea tangu mwaka 1989 ambapo kimbunga kama hicho kilitokea na kuua zaidi ya watu 400 na mwaka 1962 kiliua watu 900
Surat thani ni eneo ambalo linajulikana sana kwa utalii vikiwemo visiwa maarufu kama Koh Samui, Koh Tao na Koh Phangan.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.