UNUNUZI WA ZAO LA KOROSHO BADO NI KITENDAWILI

Umefanyika Mnada mwingine wa korosho November 4,chini ya usimamizi wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI katika kijiji cha Mnero Ngongo wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Kati ya Zaidi Ya Tani Elfu tisa zilizopigwa mnada,ni Tani 50 tu zimeuzwa na wakulima wa Ruangwa,Nachingwea na Liwale kwa bei ya Tsh.3001 kwa kila Kilo.

Kampuni moja ya Korosho Africa pekee imejitokeza kununua, huku mwenyekiti CBT,Mama Anna Abdallah akigusia mpango wa wabanguaji kuruhusiwa minadani ili wanunue korosho kwa bei ya juu ya mnada husika.

Bado wakulima wanaendelea kulalamikia kinachoendelea kwani ni wazi siku zinakwenda na wanunuzi wanajitokeza wachache na kununua korosho chache.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.