UNILEVER TANZANIA LTD YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA ‘ONJA LADHA USHINDE’

Kampuni ya Unilever Tanzania Limited, Siku ya jana  Julai 10, 2018 imekabidhi zawadi kwa washindi wanne kati ya sita walioibuka kidedea katika  promosheni ya Onja Ladha Ushinde.

Akikabidhi zawadi hizo Meneja wa Fedha wa Kampuni hiyo, Raymond Antony amewataja washindi hao kuwa ni pamoja na Kenedy Wilfred na Himida ambao kila mmoja amejinyakulia kitita cha shilingi 50,000/=, huku washindi wengine Upendo Frank kutoka Sayansi Kijitonyama na Godfrey Francis kutoka Kisutu wakijishindia Mbuzi kwa kila mmoja.

Meneja wa Fedha Raymond Antony akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa Upendo Frank kutoka Kijitonyama

Akieleza sababu ya kuanzishwa kwa promosheni hiyo, Raymond amesema wameamua kurudisha faida ya kile kinachopatikana katika kampuni yao kwa jamii, maana wao kama Unilever Tanzania Ltd bidhaa zao zinagusa jamii na hivyo ni jambo la busara kurudisha fadhira kwa wateja wao.

Meneja wa Fedha Raymond Antony akikabidhi zawadi ya pesa taslimu 50,000/= kwa mshindi Kenedy Wilfred

Kwa upande wao washindi wa promosheni hiyo hawakusita kueleza furaha yao baada ya kupokea zawadi hizo, huku wakidai kuwa walikuwa hawaamini kama kweli shindano hilo ni lakweli maana kumekuwepo na maneno mtaani kuwa washindi huandaliwa na kuwa zawadi huwa ni za kujuana.

Godfrey Francis akielezea furaha yake mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya mbuzi, huku akiwashukuru Unilever Tanzania Ltd kwa zawadi hiyo

“Nampeleka huyu mbuzi hadi kazini kwangu maana kuna wenzangu hawakuamini kama kweli zawadi hizi zinatolewa”, alisema Godfrey Francis aliyejishindia mbuzi.

Aidha washindi wa zawadi hizo wamesema pia watakuwa mabalozi kwa watu wengine baada ya kujiridhisha kuwa ni kweli zawadi hizo zinatolewa bila upendeleo wowote.

Meneja Masoko wa Unilever, Lumuli Minga (wa kwanza kushoto) akitoa pongezi zake kwa washindi.

Naye Meneja Masoko wa Unilever, Lumuli Minga, alitumia wasaa huo kuwaomba watanzania kuendelea kushiriki mara nyingi zaidi katika promosheni hiyo ili waweze kuibuka washindi, huku akiwapongeza wale wote waliokabidhiwa zawadi.

Moja ya pack za Promosheni zikiwa na stika kama zinavyoonekana kwenye picha

Jinsi ya kushiriki promosheni ya ‘Onja Ladha Ushinde’ unatakiwa kununua bidhaa za Royco 200g au 10g, au Bleu Band 500g au 1kg zenye stika ya promosheni kisha kwangua namba za siri na ukimaliza tuma namba hizo kwenda namba 0683666888 ambapo utapokea ujumbe mfupi ukikujulisha kuwa umeingia kwenye droo ya shindano hilo.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.