UKIMSHIKA HAPA AUNT EZEKIEL USHAMMALIZA

SUPASTAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amesema kama unataka kumjua upande wake wa pili wa shilingi, jaribu kuyafuatilia mapenzi yake na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ambaye ni dansa wa kutegemewa katika Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), utakiona cha mtemakuni.

“Hivi kwa nini uhangaike kuyajua maisha yangu na mpenzi wangu? Leo tumegombana au tumepatana au tunaelekea kuachana, inakuhusu nini wewe? Maana hata tulivyoanza uhusiano watu walishtukizia tuko kwenye uhusiano hivyo hata kama tukiachana wataona hivyohivyo,” alisema wakati akizungumza na Ijumaa hivi karibuni.
Aliongeza:
“Nimekuwa nikisikia minon’gono mingi kuhusu kuachana na Iyobo, lakini ukweli ni kwamba siku tukiachana hakuna mtu atajua labda kila mtu atakapomuona mwenzake na mtu mwingine maana nimechoka kuchunguzwa kila wakati kuhusu penzi langu.”

Aunt Ezekiel ameonekana kufanya vizuri kwenye filamu hasa akicheza na Mboto na kumfanya kuwa miungoni mwa wasanii pendwa

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.