UFARANSA YAIKABIDHI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI SILAHA ZA KIVITA ZAIDI YA 1,400

Bangui, AFRIKA YA KATI.

Serikali ya Ufaransa juma hili imekabidhi bunduki zaidi ya elfu 1,400 aina ya AK-47 kwa vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati vinavyokabiliana na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly, alishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye kambi ya jeshi ya M’Polo iliyoko mjini Bangui.

Msaada huu wa kijeshi ni sehemu ya ahadi ya Serikali ya Ufaransa iliyoitoa mwezi Novemba jijini Paris, sambamba na euro milioni 24 kama msaada wa kibinadamu.

Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamepoteza maisha katika mapigano huku wengine zaidi ya laki 7 wakiwa ni wakimbizi wa ndani na wengine zaidi ya laki 5 wakiikimbia nchi yao.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.