UCHAFU WA SOKO LA MPWAPWA, TISHIO KWA AFYA ZA WANANCHI

Mpwapwa -Dodoma

Uchafu uliokithiri Katika maeneo ya soko la Mpwapwa pamoja na maeneo ya migahawa ya Mti mkuu umetajwa kutishia afya za wananchi wakihofia kutokea kwa magojwa ya mlipuko Katika mji huo.

Hali hiyo imebainishwa na Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM,wilaya ya Mpwapwa, Said Mguto wakati wa ziara ya ukaguzi wa Ilani ya chama cha Mapinduzi mjini hapo.

Amesema kuwa, kutokana na uhaba wa huduma za vyoo, usimamizi mbovu wa sheria ndogo za Halmashauri, harufu za rushwa na urasimu kwa baadhi ya watumishi wa serikali kumepelekea uchafu kutotolewa katika maeneo ya biashara mjini humo.

Aidha katika ziara, amejionea baadhi ya wafanya biashara wakisaidia katika makopo na kwenye kuta za vibanda vya biashara kitu ambacho kinapelekea kuwa harufu Kali na kutishia kutokea kwa magojwa ya mlipuko.

Pia kutokana na hali katibu mwenezi ameshauri kufunguliwa kwa Choo kilicho jegwa na mwekezaji bwana Emanuel Mmasi aliye amriwa kuto kuruhusu matumizi yake baada ya kubaini kukosewa kwa ramani ya jengo hilo.

Kwa Upande wake kaimu Ofisa Afya wa wilaya Bi Legina Mfungo ameshauri uongozi mji mdogo wa Mpwapwa akiwemo Mwenyekiti wa mji, Mtendaji Kata na vijiji kuweza kuruhusu Choo kilicho jengwa na mwekezaji huyo kuanza kutumika Mara moja ili kuepuka kutokea kwa magojwa ya Mlipuko wakati mmiliki huyo akikifanyia marekebisho Choo hicho.

Akifunga ziara hiyo katibu mwenezi amewataka watendaji wa serikali kuweza kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto zinazo ikabili jamii Kama anavyo agiza Mwenyekiti CCM Taifa Mhe,Dkt,John Pombe Magufuli ili kuweza kufikia uchumi wa Kati na Tanzanian ya Viwanda.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.