Takribani watu 133 wanatafutwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo kushindania kitita cha sh milioni 108 ambazo zitatolewa hapo kwa hapo kwa kila mshindi mwishoni mwa mwezi huu
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Meneja wa wateja maalumu wa Tigo Bi. Marry Rutta amesema kuwa kupitia shindano hilo watakua na droo kubwa ya kutafuta washindi 3 watakaojipatia fedha taslimu kuanzia milioni 5 hadi 15.
Aidha Bi. Rutta ameongeza kuwa kupitia mashindano hayo ya Tigo pesa washindi 4 walijipatia milioni 1 baadhi yao ni Neema Frank na Frank Guosha pia washindi 16 walijipatia laki 5 baadhi yao ni Halima Said Shabani, Fatuma Ally Machimbo na Ashura Ally Salimu.
Hata hivyo Bi. Ruta ametoa wito kwa wateja wa Tigo kuendelea kufanya miamala ya Tigo pesa ili waweze kuingizwa kwenye droo ya kujishindia pesa kuanzia laki 5 had milioni 15
Kwa upande wake meneja wa mawasiliano wa Tigo Bi. Woinde Shisaeli anawasisitiza wateja wa Tigo waendelee kufanya miamala ili waweze kufikia malengo yao.
Bi. Shisaeli alimalizia kwa kusema kuwa wameweka zawadi hizo kwa kuwashukuru wateja wao wa Tigo kwa huduma wanazozifanya kwa upande wa Tigo pesa.