THAILAND:WENGINE WANNE WAOKOLEWA KUTOKA KWENYE MAPANGO WALIYOKUWA WAMEKWAMA

Mshauri wa kamanda wa kikosi maalum cha waokoaji nchini Thailand amesema kuwa wavulana wengine wanne wametolewa nje ya pango hapo jana na hivyo kuifanya idadi ya waliookolewa kufikia vijana wanane.

Magari manne maalum ya kuwahudumia wagonjwa yalionekana yakiondoka eneo la karibu na pango lililofurika maji ambapo wavulana wa timu ya kandanda wamekuwa wamekwama kwa zaidi ya wiki mbili, hali inayodokeza kuwa jumla ya watu wanane kati ya 13 waliokwama katika pango hilo sasa wametolewa.

Hakuna taarifa rasmi kutoka serikalini kuhusu operesheni hiyo na hawajatoa taarifa kuhusu idadi ya wale ambao wametolewa pangoni. Hapo jana wavulana wanne waliokolewa. Wavulana hao walikwama ndani ya pango hilo Juni 23 baada ya mazoezi yao ya kandanda.

Related posts

One Thought to “THAILAND:WENGINE WANNE WAOKOLEWA KUTOKA KWENYE MAPANGO WALIYOKUWA WAMEKWAMA”

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.