TANZIA: MSANII JEBBY AFARIKI DUNIA.

Tasnia ya muziki hapa nchini imepata pigo jingine mara baada ya kumpoteza msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Jebby, ambaye amefariki dunia siku ya leo April 22, 2018, huko mjini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Chanzo cha kifo chake kinatajwa kuwa ni ugonjwa wa bandama, ambao kwa maelezo ya ndugu zake, umekuwa ukimsumbua kwa siku nyingi.

Marafiki zake wa karibu akiwemo msanii Afande Selle, pia amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii Jebby, ambaye amewahi kutamba na kibao chake cha ‘Swahiba’ambacho walishirikiana na Afande Selle.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.