TAHADHARI: TAREHE 27 JULAI KUSHUHUDIWA TUKIO LA KUPATWA KWA MWEZI KWA MUDA MREFU ZAIDI

Taarifa kutoka kwa Shirika la Usimamizi wa Anga za Juu (NASA) zinasema kuwa siku ya kesho kutwa Julai 27, 2018, dunia itashuhudiwa tukio la kupatwa kwa mwezi, ambalo si la kawaida.

Kwa mujibu wa habari iliyoripotiwa na BBC mapema siku ya leo inasema kuwa, shirika hilo limetoa taarifa inayosema tukio la kupatwa kwa mwezi mnamo siku hiyo ya Julai 27 litakuwa la muda mrefu zaidi kuwahi kutokea katika karne ya 21.

Kivuli cha tukio hilo kama ambavyo kitaonekana katika setilaiti

Taarifa hiyo inaeleza kuwa tukio hilo litashuhudiwa kwa ukaribu zaidi katika maeneo ya Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, katikati mwa Asia na Australia ikiwa ni maeneo yote isipokuwa kaskazini mwa Marekani.

Kivuli cha tukio hilo kitaonekana katika setilaiti bila kuziba mwangaza wote.

Tukio la Kupatwa kwa mwezi hutokea wakati jua, dunia na mwezi zinapofungamana, nah ii humaanisha kwamba dunia iko katikati ya Jua na Mwezi, kitendo kinachopelekea kuzibwa kwa mwanga wa jua na hivyo kutokea giza.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.