TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MSAADA WA VITABU CHUO CHA UUGUZI NA UKUNGA MAKANDANA.

 

Mbeya.
Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson hii leo imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 10 kwenye chuo cha Uuguzi na Ukunga cha Makandana Tukuyu wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Akikabidhi msaada huo meneja wa Tulia Trust Jacquecline Boaz, amesema msaada huo umetolewa baada ya kupokea maombi kutoka kwa uongozi wa chuo kutokana na uhaba wa vitabu vya kufundishia hususani vya sayansi ambavyo ni aghali na vingi hapatikani nchini.

Awali baadhi ya wanachuo akiwemo,Rais wa chuo hicho Asante Kalindima na makamu wake Theresia Khaday wamesema chuo kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa vitabu katika chuo hicho hali iliyopunguza ufanisi katika masomo yao.

Aidha wameishukuru taasisi ya Tulia Trust kwa kutoa msaada wa vitabu na kwamba Vitabu hivyo kwani vitawasaidia kusoma kwa hamasa kubwa na kuyafikia malengo.

Akipokea msaada huo mkuu wa chuo hicho Norasca Mtega mbali na kuipongeza taasisi ya Tulia Trust amesema msaada huo umekuja kwa wakati na kwamba umesaidia kupunguza changamoto ya vitabu.

Hata hivyo ameahidi kuvitunza ili viweze kusaidia wanachuo wengi watakaosoma katika chuo hicho.

Kabla ya kukabidhi vitabu hivyo meneja wa Tulia Trust Jacqueline Boaz alioneshwa Bweni la wanachuo lililosimama kujengwa kwa muda mrefu litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo mia moja ambapo Jacqueline amesema taasisi yake imeichukua changamoto hiyo na ataifikisha sehemu husika.

Taasisi ya Tulia Trust imekuwa ikijihusisha na utoaji wa mikopo nafuu katika wilaya ya Rungwe na Mbeya ambapo sehemu ya faida huirudisha katika huduma za kijamii kwa kutoa misaada ya elimu, afya, maji na wahitaji wengine hususani makundi maalumu yanayoishi mazingira magumu.

Taasisi hiyo ya Tulia Trust pia imetoa msaada katika chuo cha Afya na uuguzi cha St. Joseph health kilichopo Kata ya Iganzo jijini Mbeya.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.