SIMBA YAANZA NA MWADAUI YAICHAPA 3-0

Na Shabani Rapwi.

Klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) ulipigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya Simba SC kufikisha jumla ya alama 36 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na michezo 6 mkononi, ikizidiwa alama 19 na kinara wa Ligi Yanga SC aliyefikisha alama 55 katika michezo 22.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Meddie Kagera dakika ya 21′, Mzamiru Yassin dakika ya 26′ na John Bocco dakika ya 29′.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.