SIKU 7 SASA MWILI UPO MOCHWARI BILA KUTAMBULIWA NA NDUGU,JAMII YAASWA KUTEMBEA NA VITAMBULISHO

Amiry Kilagalila,Njombe.

Serikali mkoani Njombe Imewataka watanzania kujenga mazoea ya kutembea na nyaraka zote muhimu za utambulisho wao pindi eanapokuwa safarini Ili kurahisisha mawasiliano wakati linapotokea jambo lolote linalohitaji mawasiliano ya dharura.

Wito huo umetolewa na afisa ustawi wa jamii kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kibena mkoani Njombe bwana Samson Sollo Wakati akizungumza na vyombo vya habari juu Ya mkazi wa mmoja wa Songea Aliyefahamika Kwa majina ya George Lutuhi ambaye amefariki akiwa anapatiwa matibabu na hakuna ndugu aliyejitokeza hadi sasa.

“Nauomba umma kuweza kutusaidia kuwapata ndugu wa marehemu George Lutumo,ambaye ni mkazi wa Songea alikuwa ni mvuvi alikuwa akisafiri kuelekea Mtera mkoani Iringa siku ya tarehe moja mnamo saa moja na nusu asubuhi tuliweza kumpokea hapa hospitalini kutoka katika gesti aliyokuwa amepumzika na tumeweza kumuhumia lakini kwa bahati mbaya aliweza kupoteza maisha na tuliweza kutafuta taarifa zake hatukuweza kufanikiwa”alisema afisa afya.

Bwana Sollo amesema marehemu baada ya kuugua alifikishwa hospitalini hapo na wasamalia disemba mosi ya mwaka huu akitokea katika nyumba ya kulala wageni ya Iditima iliyopo mjini Njombe Eneo alilofikia kabla ya kuelekea Mtera Huko mkoani Iringa kwenye shughuli za uvuvi.

Aidha afisa ustawi huyo amesema taarifa za Alawali walizipata katika nyumba hiyo ya wageni alikofikia kabla ya umauti kumkuta lakini kwa bahati mbaya hakukutwa na simu,taarifa zozote Wala nyaraka muhimu za utambulisho jambo ambalo limewalazimu kutumia vyombo Vya habari kutoa taarifa Hiyo.

Alfred Melele ni Daktari atika hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe ya Kibena ambaye amesema marehemu anakadiriwa kuwa na umri wa mkaka 29 hadi 30 na alifariki majira ya mchana siku Hiyo Hiyo ya Disemba mosi.

“tulipima vipimo vyote kwenye damu,sukari pia ilikuwa kawaida kipimo cha malaria kipimo cha virusi lakini marehemu alikuwa anatoa harufu mdomoni kama alikuwa amekunywa pombe sana na kuonekana kama alikuwa anatumia vidonge vya Parasetum inawezekana alikuwa anaumwa mda mrefu kwa hiyo alikuwa anatumia dawa na akatumia vinywaji vikampelekea kuto kujitambua na kuwa na hali mbaya”alisema daktari Melele

Dokta Melele amesema kwa mujibu wa taratibu ndugu wasipopatikana katika kipindi cha siiku 14 Kuchukua mwili huo basi serikali italazimika kuuzika.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.