SHAMBULIO LA AIBU LAMFIKISHA MAHAKAMANI MWINGINE ASHITAKIWA KWA KUJARIBU KUBAKA

Watu wawili wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Serengeti kujibu mashtaka katika kesi mbili tofauti mmoja akijaribu kubaka na mwingine akifanya shambulio la Aibu

Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Renatus Zakeo alisema katika shauri la jinai namba 2/2019 mshitakiwa Manyama Machota(36) mkazi wa kijiji cha Robanda wilayani hapa anashitakiwa kwa kosa moja la Shambulio la aibu

Zakeo alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 9 mwaka 2018 katika kijiji cha Robanda baada ya kumshika binti aitwaye Zawadi Peter(16) sehemu mbalimbali za mwili wake bila ridhaa yake kosa ambalo ni kinyume na kifungu 135(1)cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Mshitakiwa aliomba dhamana na mahakama ilitoa masharti ya kuwa na wadhamini wawili na watakaosaini dhamana ya mdomo shilingi milioni 5 lakini mshitakiwa huyo alishindwa masharti hayo kwa kukosa wadhamini hali iliyompelekea kupelekwa mahabusu

Baada ya kusomewa mashtaka mshitakiwa alipoulizwa kama alitenda kosa hilo au lah! alikana baada ya kukana kosa mwendesha mashtaka alisema upelezi wa kesi umekamilika hivyo ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali(Ph)

Hakimu Ngaile ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 22 mwaka huu itakapoletwa kwa ajili ya kusomwa maelezo ya awali

Katika shauri la Jinai namba 3/2019 mshitakiwa Maitari Nyamako(33) mkazi wa kijiji cha majimoto amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa moja la kutaka kujaribu kubaka

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Renatus Zakeo alisema mnamo Oktoba 12 mwaka 2018 katika kijiji cha majimoto mshitakiwa alijaribu kumbaka Mariam Maitari(35) bila ridhaa yake kosa ambalo ni kinyume na kifungu 132(1)cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Hata hivyo baada ya kusomewa mashtaka mshitakiwa alikana na upelezi wa kesi bado haujakamilika Hakimu Ngaile ameahirisha kesi hiyo hadi Januri 22 itakapotajwa tena na mshtakiwa amepelekwa mahabusu

Wakati huo huo washitakiwa saba katika shauri la Uhujumu uchumi namba 74/2018 wameahirishiwa kesi yao hadi ifikapo Januari 22/2019 itakapoendelea kusikilizwa katika hatua ya ushahidi

Akiomba ahirisho mbele ya Hakimu Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Elisa Benjamini alisema kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa kwa shahidi mmoja wa mwisho lakini ameomba ipangwe tarehe nyingine kwa sababu Jarada la washitakiwa bado lipo mkoani kwa mwanasheria wa Serikali

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Yohana Nyambeo(45) Peter Kongoli(38) Mayonga Hamisi(41) Jummatano Boniphace(35) Wangi Samwel(38) Joseph Nyambacha(41) na Tatu Machota(47)

Kwa pamoja wanashitakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuingia ndani ya Hifadhi bila kuwa na kibali,kupatikana na silaha ndani ya hifadhi,Kumiliki Nyara za Serikali bila kibali,kujihusisha na biashara ya nyara za serikali pamoja na kushindwa kutoa ripoti ya kuwepo kwa nyara za Serikali

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.