SERIKALI YAPANIA KUONGEZA AJIRA KUPITIA VIWANDA.

Iringa. Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli, imepania kuongeza ajira kwa watanzania kupitia sekta ya viwanda hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo mjini Iringa, na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la kitaifa la Viwanda lililofanyika katika Ukumbi wa Kichangani mjini Iringa.

Mwijage amesema kuwa nia ya serikali ni kuongeza ajira kwa watanzania kupitia sekta ya viwanda, ambapo amewasisitiza viongozi wote katika ngazi za mikoa na wilaya kutenga maeneo kwaajili ya ujenzi wa viwanda.

Waziri Mwijage pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wapo mkoani Iringa kwaajili ya maandalizi ya kuelekea Siku ya Wafanyakazi Duniani, maarufu kama ‘Mei Mosi’, ambayo mwaka huu maadhimisho yake kitaifa yatafanyikia mkoani humo.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.