SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YACHUKIZWA NA WAFANYABIASHARA

Zanzibar, Mjini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 11 wa Jumuiya Ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda Na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA). Uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Malindi mjini Zanzibar

Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif alieleza, Serikali makini husisitiza umuhimu wa jumuiya ya Wafanyabiashara yenye kuleta manufaa na faida kwa kufungua milango ya biashara ndani na nje ya nchi

Sambamba na kuongeza wigo wa pato la Taifa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachukizwa na kuona watu wachache wanaigeuza sekta ya biashara kuwa kichaka cha wakwepa kodi, wala rushwa na waingiza bidhaa za magendo.

Aliongeza wapo Wafanyabiashara wachache wasiojielewa kiasi cha kufanya mambo hayo ambayo ni kinyume na sheria, huku wengine wakiingiza bidhaa zisizo na ubora na kuuza kwa bei ya juu.

Balozi Seif amewaasa Wafanyabiashara kuwa makini, na kufahamisha kuwa wakati umefika kwa Wafanyabiashara nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata maadili, sheria na uadilifu. Hali ambayo italeta manufaa makubwa kwa nchi na Wananchi.

Balozi Seif aliuagiza uongozi wa ZNCCIA, kuhakikisha inawajengea uwezo Wafanyabiashara wa Zanzibar ili waweze kutekeleza majukumu kwa weledi na kwenda sambamba na mabadiliko ya kidunia.

Alieleza kua nafasi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara katika maendeleo ya Nchi kiuchumi haina mjadala na uimara wake utatokana na wanachama walio hai watakaochangia ujenzi wa uchumi wa Nchi.

Alisema ni faraja kwa Serikali kuona Taasisi hiyo inayosimamia mazingira ya Biashara Nchini inaendelea kuwa mlezi mzuri wa wazalishaji wadogo wadogo na Wakulima ili lengo la kuwa katika Nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020 lifanikiwe.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.