SERIKALI YA MAGUFULI YASITISHA TENA AJIRA HIZI,

 

 

NA KAROLI VINSENT

WAKATI idadi ya wahitimu wa Chuo Kikuu kukosa ajira likiwa limeongezeka kwa kasi nchi kwa sasa kutokana na masuala mbali mbali ikiwemo hali ya uchumi iliyopelekea makampuni mengi kupunguza wafanyakazi ili yaweze kujiendesha kutokana na hali ilivyo.

Wakati hayo yakiendelea Serikali ya Rais John Magufuli yatangaza kusitisha ajira tena mbapo sasa  imesitisha kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii kupitia mradi wa Global Fund na badala yake imesema inaelekeza nguvu kuajiri watumishi kwenye sekta ya afya.

Usitishaji huu wa Ajira ni wa Mara ya pili ambapo mwaka 2016 serikali ilitangaza kusitisha ajira nchi nzima kwa kile ilichodai kupisha zoezi la uhakiki .

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege alisema hayo baada ya kuwapo kwa barua inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayotoka Tamisemi ikielekezwa kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbeya na Chunya, ikimtaka kusitisha ajira hizo.

 

Kandege alisema Wizara ya Afya inajenga vituo vya afya na zahanati nyingi vijijini na mijini, hivyo ina uhitaji mkubwa wa wahudumu wa afya.

 

“Tukiwaajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii huku zahanati na vituo vya afya tulivyojenga vina ubora na uwezo wa kutoa huduma kubwa ikiwamo upasuaji, ina maana tulichofanya itakuwa kazi bure,” alisema

 

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chunya mkoani Mbeya, Sophia Kumbuli alisema kulikuwa na mchakato unaendelea wa kutaka kuajiri watu wa kada hiyo, lakini suala la kusitishwa hana taarifa nalo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.