SASA ZAMU YA WAKUU WA WILAYA, RAIS MAGUFULI AMTUMBUA DC KAHAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ametangaza kumfuta kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ndugu Fadhili Nkurlu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu zinasema kuwa, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo hii leo Julai 15, 2018.

Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

Mkuu wa Wilaya, Anamringi Macha ametakiwa kuripoti katika kituo chake cha kazi mara moja.

Hata hivyo taarifa hiyo haijaeleza sababu za Rais Magufuli kufikia uamuzi wake wa kumtumbua ndugu Fadhili Nkurlu.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.