SALUM MWALIM:OLENASHA ALIOMBE RADHI TAIFA.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Zanzibar Salum Mwalimu amemtaka naibu waziri wa elimu William Olenasha kujitokeza na kuliomba taifa radhi kutokana na kauli yake ya kuwa mawaziri hawaendi kwenye majimbo ya wapinzani(wahuni)

Mwalimu ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho mjini Njombe.

“Juzi nimeona naibu waziri mmoja bila aibu anazungumza mambo ya ajabu eti pale nilikuwa siji mlikuwa mnanialika kwasababu mbunge wenu hapa alikuwa ni CHADEMA,Olenasha atoke aliombe taifa radhi unaibu waziri sio wakwake wala sio wa baba yake ni wa watanzania wote bila kujali itakadi za vyama vya siasa yaani kiongozi wa kitaifa unaligawa taifa kwa misingi ya itikadi hapa ndio tulipofikishwa huku ni kulewa madaraka”amesemMwalimu.

Aidha amemtaka katibu mkuu kiongozi ajitokeze na kukemea kauli ya waziri huyo.

“Tunamuommba katibu mkuu atoke akemee alaani kauri ya naibu Waziri na naibu waziri awajibishwe juu ya kauli hiyo,tunataka taifa lenye umoja na mshikamano na tunataka viongozi wanaotuunganisha watanzinia sio kutugawa, kwa namna yoyote ile sisi tutasema na huo ndio wajibu wetu”ameongeza Mwalimu.

Siku mbili zilizopita kumekuwa na video inayozunguka mitandaoni ikimuonyesha naibu waziri huyo akiwa na mbunge wa simanjiro James Millya na kusikika akisema kuwa mawaziri hawaendi kwenye majimbo ya upinzani kwa kuwa ni chama cha wahuni.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.